Mwakilishi wa heshima wa Tanzania, Balozi Johan ambae aliwahi pia kuwa Balozi wa Jamhuri ya Korea Kusini akimpa maelezo Mhe. Naibu Spika, Job Ndugai wakati alipomtembeza katika jengo lenye historia ya waliowahi kuwa wafalme wa Korea. Nchi hiyo iliamua kuondokana na utawala wa kifalme na kuwa Jamhuri. Mwaka 2012 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Desemba.
Mhe. Naibu Spika Job Ndugai akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu vyakula vya asili vya watu wa Korea wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshima yake na Balozi Johan. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea, Bi. Hahn. Wa kwanza kulia ni Ndugu Athuman Kwikima, Afisa Tawala katika Ofisi ya Bunge alieko masomoni katika Chuo Kikuu cha Seoul nchini humo.
Mhe. Naibu Spika, Job Ndugai akiwa katika mazungumzo na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Korea Kusini alipokutana nao muda mfupi kabla ya kukutana na Watanzania waishio nchini humo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Watanzania waishio nchini Korea Kusini, Bw. Msofu akimkabidhi Mhe. Naibu Spika risala ya wanajumuiya hao ili aweze kuifanyia kazi mara baada ya kuisoma mbele yake.
Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Judith anaesoma nchini Korea akimuuliza swali Mhe. Naibu Spika Job Ndugai mara baada ya Naibu Spika huyo kuwahutubia watanzania waishio nchini Korea. Mhe. Naibu Spika alihitimisha ziara yake mwishoni mwa wiki.PICHA ZOTE NA SAIDI YAKUBU WA OFISI YA BUNGE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2012

    God bless Tanzania, hizi safari za hawa waheshimiwas zina faida yeyote kwa nchi? Do they provide any reports when they come back - I mean a published one which can be read by wananchi?

    Naona viongozi ni kama wanashindana mahali pa kwenda.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2012

    All developed countries have so many problems eg unemployment etc, I am not sure if they happy at all entertaining viongozi continuously wanaomba misaada, 50 years baada ya Uhuru

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...