Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi akimkabidhi vifaa vya huduma na tiba, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Kimara, Dk. Alphoncina Mbinda katika hafla maalum iliyofanyika jana, kwenye Zahanati hiyo, Kimara, Dar es Salaam. Vifaa hivyo vya sh. milioni 5.1, vimepatikana kutokana na michango ya wanachama na viongozi wa Jumuia ya Wazazi Tanzania. Wengine katika picha ni baadhi ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi, Katibu Mkuu Hamis Dadi (kulia) Katibu Wilaya ya Kinondoni, Stanley Mkandawile (wapili kulia), na katikati ya Makamu na Mganga Mfawidhi ni Kaimu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dogo Mabrouk.
Wana-CCM Kata ya Kimara wakishangilia wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wanachama wa Jumuia ya Wazazi waliohudhuria sherehe hiyo.
Wana-CCM na wananchi kwa jumla wakijimwaya mwaya kucheza muziki wa taarab, kushangilia makabidhiano ya vifaa hivyo vya huduma na tiba kwa Zahanati yao.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye sherehe hiyo ya makabidhiano ya vifaa vya huduma na tiba kwa Zahanati ya Kimara. Kulia (Mwenye koti) ni Diwani wa Kata hiyo ya Kimara kwa tiketi ya Chadema.Picha na Bashir Nkoromo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2012

    Michuzi wacha uchokozi, zanzibara? sawa bwana!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2012

    C.C.M Hoyeeee Ndani ya Kimara!!!

    CHADEMA Ziiiiiiiii !!!

    Ohhh Kimara ni ya Wachagga na Chadema ndio Chama cha kila Mchagga, nani kasema hivyo?

    Mpo wapi sasa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...