Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Khamis Kagasheki  akizungumza wakati akizindua rasmi Baraza jipya la wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambalo lilichaguliwa na wawakilishi wa wafanyakazi katika mkutano wa 19 wa baraza hilo unaoendelea mjini Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Maimuna Tarishi akizungumza wakati akikimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Khamis Kagasheki.
wajumbe wakimsikiliza Waziri Kagasheki wakati akifungua mkutano.
Waziri wa Maliasili na Utalii mhe. Khamis Kagasheki akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza baada ya kulizindua rasmi baraza hilo.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Khamis Kagasheki amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za utendaji wa kazi na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa.

Rai hiyo ameitoa mjini Morogoro wakati akizindua rasmi Baraza jipya la wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambalo lilichaguliwa na wawakilishi wa wafanyakazi katika mkutano wa 19 wa baraza hilo unaoendelea mjini Morogoro.

Mhe. Waziri aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kuwa kama wafanyakazi wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutekeleza wajibu wao kama wawakilishi na kuwataka kufikisha ujumbe kwa wawakilsihi wao ili kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji kazi huku wakitoa kipaumbele kwa maslahi ya Taifa.

“Moja ya changamoto kwa Baraza hili ni kutekeleza wajibu wenu wa uwakilishi kwa uhakika. Mrudipo vituoni fikisheni ujumbe wa Baraza kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za utendaji wa kazi. Mkitekeleza wajibu wenu kama Wajumbe wa Baraza, mtarahisisha kazi ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara”, alisema Waziri Kagasheki.

Pia aliwataka watumishi katika kutekeleza majukumu yao kuhakikisha wanaimarisha ushirikiano, utendaji kazi kama timu moja kuwa wazi na kuaminiana hususan katika maamuzi yanayohusu wengi.

Aidha, katika utekelezaji wa majukumu yenu, mnapaswa kuimarisha ushirikiano, utendaji kazi kama timu moja kwa uwazi na kuaminiana hususan katika maamuzi yanayohusu wengi. Wakati wote mnapotekeleza haya, zingatieni kutanguliza mbele maslahi ya Taifa”, alisema Waziri Kagasheki.

Alisema kwamba anaimani kuwa wafanyakazi hao wataendelea kudumisha kasi ya utendaji kazi wa Wizara kwa ufanisi mkubwa huku wakizingatia umuhimu wa vikao vya baraza hilo na kutoa fursa sawa ya kushiriki majadiliano wawakilishi wa wafanyakazi.

Awali akimkaribisha Mhe. Waziri , Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bibi Maimuna Tarishi alisema kufanyika kwa mkutano huo ni kutekeleza azma ya serikali ya kuimarisha utendaji kazi wa Wizara kwa kukaa pamoja baina ya wawakilsihi wa wafanyakazi na uongozi wa Wizara na kujadili masuala ya kiutendaji yanayoihusu wizara ili kupiga hatua za kiutendaji.

Katika mkutano huo wa 19 wa baraza hilo unaofanyika Mjini Morogoro kuanzia Julai 31 hadi Agosti 1, bi Bure Nasibu alichaguliwa kuendelea kuwa katibu wa baraza hilo kwa kura 31 na Bernard Urassa kuwa katibu msaidizi kwa kura 7.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2012

    Picha ya pili kutoka chini naona jamaa ana 'ze leboz' kwenye suti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...