RASTEMWI PRODUCTIONS yenye makao yake jijini Dar es Salaam itaingiza sokoni filamu yake mpya inayoenda kwa jina la wrong LANE ‘njia POTOFU’ wakati wowote kuanzia sasa.
Mkurugenzi mtendaji wa RASTEMWI PRODUCTIONS, Dr. Rama Mwiru, amesema filamu hiyo imeshirikisha wacheza filamu nyota wa Tanzania kama Miriam Jolwa ‘jini kabula’, Rose Michael ‘zambarau’, Gilbert Sindani ‘mack’, Ibrahim Banane ‘mzee katembo’, na Kulwa Kikumba ‘dude aka Dr lugusha’. Ma-star wengine walioshiriki kwenye wrong LANE ni pamoja na Salma Jabu ‘Nisha’, Mariam Mndeme, Kojack Chillo, Michael Philipo ‘kojack’, Alice Bagenzi ‘rayuu’, Mustafa Matambo na mwanamuziki maarufu wa zouk Rehema Tajiri.
Filamu ya wrong LANE pia inaingia sokoni ikiwa imeshirikisha wacheza filamu wapya na wenye vipaji vya hali ya juu kama Salma Tuesday ‘salma chuzi’ ambaye ni mtoto wa ma-supa stars wa bongo movie, Mr. Chuzi na Kabula. Wengine wageni lakini wenye vipaji vya hali ya juu ni Dhahabu Francis, Johnson George ‘john cena’, Salvina Stambuli, Mohamedy Ally, Fadhil, na Dr. Rama mwenyewe.
Dr. Rama amesema wrong LANE imelenga kuwaburudisha na kuwapa mafunzo mbalimbali ya kimaisha watanzania na watu wengine wanaopenda filamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...