Uncle nimeona nishare hii na wadau wengine ya jinsi ma-Flyovers yalivyo jijini Nairobi, Kenya. Hivi tanzania tutafika hapa lini hapa,au ndo maneno mengi vitendo zero?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Sisi bado tupo tupo kwanza.

    ReplyDelete
  2. Great!! Na hii ikifika hapa kwetu itabindi madereva waanze kufundishwa upya jinsi ya kuendesha kwenye barabara za kistaarabu. Maana hapa mjini kila dereva anaendesha utafikiri anatembea kwa miguu, mara kachomeka huku, mara huku, anajifanya ana haraka. Haraka yenyewe sio kwamba anawahi ofisini, bali baa, au kwingine kwa ajabu.

    La sivyo, itakuwa ring-roads zinatupeleka lkwenye ring-deaths!! Let's be civilised Bongo-men (I mean men, women are better behind the wheel).

    ReplyDelete
  3. Hadi kizazi cha kifisadi kipite, tupate wazalendo ndipo maendeleo yatakuwepo.

    ReplyDelete
  4. Pamoja na hizo barabara mpya hawajaweza kumaliza tatizo la foleni. Dar wakiweza hizo barabara za mabasi yaendayo kasi, treni na feri kwa tegeta na bunju, hata hao watani watatutamani wenyewe.

    ReplyDelete
  5. duh !!! kwanza umenitisha ,nilifikili picha umepiga UK !!! Mungu wee !! mbona tuko nyuma namna hii ?? ujanja wa maneno tu na WIZI, huko hatutafika,kamwe. Kama pesa zinachukuliwa na kufichwa Swiss bank, au hayo majizi kwa jina la ( mafisadi) yanajilimbikiza majumba ya kifahari na mitoto ya mijizi hayo iko Ulaya inatanua na magari ya bei mbaya, je ?? hiyo hela ya kununulia lami itatoka wapi ???.Huyo karani tu wa tannesco ana nyumba 3 je ? huyo boss wake anazo ngapi ?? halafu ukimfikia huyo waziri wa hiyo wizara ndipo utakaposhika adabu yako.Cha ajabu, hayo hayo majizi,tunapanga nayo foleni kwenye barabara zetu mbovu, ha ha ha patamu hapo. Kenya kuacheni kama Kenya-wenzetu wanapochoshwa ,huwa wanatumia mapanga .Sisi watu wa amani,mimi niko upande wa amani kuliko haya mafly over au umeme. Mdau Moshi

    ReplyDelete
  6. kuhesabiwa kwenyewe watu hawataki,hiyo nchi kweli hiyo,seti tupu, seti isiyokua na rula wala kompasi ndani yake ha ahaaaa

    ReplyDelete
  7. Tatizo waBongo hatuna utamaduni wa kusafiri.

    Nairobi ipo juu tuache ubishi na unafiki, hivyo huwezi kufananisha Nairobi na Dar Es Salaam.

    Dar Es Salaam njia ya Mbagala imetutoa kamasi ujenzi chini ya kiwango na sasa imevunjwa inarudiwa.

    Ujenzi wenyewe wa kurudia Mkandarasi anatumia (Human Labor) yaani ujenzi wa Mafundi wa mikono badala ya (Machine Automation).

    Mpaka MAFISADI WA EPA WANYONGWE NA MAFISADI WENGINE WOTE NDIO TUFIKE HUKO.

    ReplyDelete
  8. HAHAHA HUKO BADO KABISAAAA HATUJAKUFIKIA

    KWANZA TUPAMBANE NA MAFRIJI YETU NA TV ZETU ZITUMIKE VIZURI KWA KUPATA UMEME WA KUTOSHA ALAFU TUTAANGALIA HAYO MENGINE

    SUALA LA MAJI NA UMEME NI AIBU KUBWA SANA KWA NCHI KAMA TANZANIA INAYOJIGAMBA KUWA INA MAENDELEO

    UMEME NA MAJI NI VITU VILIVYOSAHAULIWA KABISA KWA NCHI ZILIZOENDELEA LEO HII TANZANIA NDIO KWANZA TUNATESEKA KWA HUDUMA HIYO

    JIANDIKISHENI SENSA MPATE KUJULIKANA IDADI YENU HUENDA MKAPATA MAENDELEO KAMA HAYO.

    ReplyDelete
  9. Kenya ufisadi upo lakini maendeleo kwa umma yapo. Bongo ni ufisadi na kujenga magorofa ya watu binafsi ndio mnaweza.

    ReplyDelete
  10. kalabwagilaAugust 28, 2012

    duh! kwanza maeneo ya makaburi itabidi yaongezwe, maana madereva wengi hapa hawajui sheria, watamwagika kweli! akikanyaga accelerator na break kajiona mtaalamu, mifano mizuri iko kwenye round-about (keep left) kinachotokea pale ni ujanja kuwahi!

    ReplyDelete
  11. Hujafika Manzese weye? Kuna flyover pale ati!

    ReplyDelete
  12. Kariakoo mifereji imejaa na imezibuka hadi vinyesi nje nje!

    Baadhi ya maghorofa yamejengwa chini ya kiwango,,,mfuko mmoja wa simenti tofali 150 badala ya tofali 15!!!

    Baadhi ya maghorofa unakuta mabomba ya maji safi yanatiririsha maji taka hadi kinyesi!

    Makandarasi wa Ujenzi eneo la Kariakoo, unakuta kampuni kama hizi DUNDULIZA CONTRACTORS LTD.,,,NDUGU YANGU BUILDERS CO. LTD.,,,KWETU MTWARA CONSTRUCTION LTD. hakuna fair bidding inayozingatia ushindani na viwango ktk mchakato wa kuwapata wajezi zaidi n.k.

    Kwa mtu mwenye akili inabidi akipangisha akae na 'miamvuli ya dharura' ama 'life jackets' kama abiria wa ndege.

    Kwa kuwa muda wowote ghorofa linaweza kuporomoka!!!

    ReplyDelete
  13. Hayo ni maendeleo makubwa tu. Lakini sisi tunalaumu viongozi tu wenyewe hatujiangalii. Linapotekea jambo badala ya kujadili chanzo tunajadili matokea yake bila kuangalia nini kimesababisha na kinatatuliwaje. Na tubadilike sisi sote sio viongozi tu. Ushabiki na unazi kwa kila kitu havitusaidii. Kwa kuwa viongozi wetu wanatoka kwenye jamii ya kikasuku tusitemee chiriku!

    Sesophy

    ReplyDelete
  14. TUTFIKA SOON,MAANA SISI TUPO IN LOCK- STEP NA KENYA: WAKIANDIKA KATIBA WAKIMALIZA NA SISI TUNAANZA, WAKIBADILISHA CHAMA KINACHOTAWALA NA SISI TUNAFUATA, WAKIJENGA BARABARA NA SISI TUTAFUATA.............

    ReplyDelete
  15. Tatizo bongo kila kitu ni dili na watu wa mipango miji wanabandika na kubandua majumba .Yaani mji hauna nafasi ya expansion wala Parks , viwanja vya michezo.Nataka nione mradi wa rapid bus transit kuanzia morroco kuja mjini na Akiba kuja posta watajenga jengaje

    ReplyDelete
  16. Ngoja tetemeko la ardhi liikumbe Nairobi tuone kama wataweza kuijenga hiyo fly-over/by-pass upya.

    Kuna ule usemi 'Iga Ufe', siye Bandari-Salama mambo yetu ni barabara za chini kwa chini kwa ajili ya Mabasi ya Kasi na usafiri kwa reli juu ya ardhi mjini.

    Hatutaki 'Iga- Ufe' kama jiji la Nairobi.

    Mdau
    Manzese Darajani.

    ReplyDelete
  17. Wadau msikate tamaa jamani. Kiukweli, kama spidi ya kukomesha mafisadi itaendelea, mbona haya masuala ya fly-overs ni kitu cha dakika tu kwetu???

    Hivi mnaonaje kasi ya ujenzi wa barabara ya Morogoro (toka Fire hadi Ubungo)??? mwaka jana kama saa hizi, nani alijua kama tungeona Ujenzi wenye kasi vile kwenye barabara hiyo na ile ya Mwenge-Tegeta na ile ya Kilwa Road?

    Kama hawa Waheshimiwa "original" (kina Mwakyembe, Magufuli, Kagasheki na Tibaijuka) wataendelea na kasi zao za kusimamia majukumu yao, nawaambia miaka mitano ijayo, Nairobi itakuwa "cha mtoto"!!!

    Just imagine, wakati huo daraja la Kigamboni likiwa limekamilika, barabara zote nilizotaja hapo juu zikiwa zimekamilika, with a few but beautifully designed fly-overs, nawaambia hii Dar hii hii, mtaitaka......

    Mungu ibariki TZ, amen.

    ReplyDelete
  18. pamoja na flyover, Nairobi ni mji wa slums Dar hamna. Kumbe wengi humu hata kusafiri kutoka dar hamjatoka. Mnastaajabu Nairobi kuwa hivi. Mji huu uliendezwa na wakoloni kwa sababu walikuwa hawataki kuongoka. Mmeshaenda Maputo mkauona mji ulivyoendelea. Ah watanzania mmelala sana.

    ReplyDelete
  19. Wapeni Uraisi Wapinzani Watawajengea Fly Over karibia kila Mji. Miaka 50 ya uhuru tumebaki na Amani(Utulivu) Tujivunieni Amani na Utulivu..Maana yake endeleeni kuwa wa Pole Mafisadi Wale wao tuu..Daa Politics is a dirty game and we are playing it.

    ReplyDelete
  20. Kwa kweli hata mimi nilidhani ni pembezoni mwa Los Angeles, maana katikati ya Los Angeles panatisha kama ni flyovers.
    Hongera Kibaki.

    ReplyDelete
  21. Maendeleo na Mabadiliko nchini Tanzania yatapatikana endapo:

    (1.)Tutaacha utamaduni wa ubinafsi kulindana, wizi na ufisadi.

    (2.)Tutajenga utamaduni wa kuulizana, uwazi na kuwajibishana miongoni mwetu.

    (3.)Tutaendesha mambo kwa vigezo na ushindani badala ya upendeleo na mipango mipango.

    BILA YA HAYO MATATU DAIMA TUTAYASIKIA MAENDELEO KWA WENZETU !!!

    ReplyDelete
  22. Wewe mdau unaosema nairobi ni mji wa slums acha ujinga. Ni kweli wana slums lakini kimaendeleo nairobi huwezi kuifananisha na Dar hata iweje, Michuzi nadanganya? Nairobi kumeendelea sana, na msije shangaa baada ya miaka 5 ijayo Kigali ikaipita Dar kwa maendeleo. Hapa Bongo tumelala sana. Tunahitaji mapinduzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...