Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(kushoto) na Balozi wa Ujerumani nchini Kluas Peter Brandes (kulia) wakisaini mkataba wa msaada wa miaka mitatu leo mjini Dar es salaam ambapo Ujerumani itaipatia Tanzania msaada wa Shilingi bilioni 352 . Msaada huo utasaidia kuboresha utawala bora katika serikali za mitaa, sekta ya afya , nishati , maliasili, maji, mfuko wa bajeti ya Serikali na kuboresha programu ya usimamizi wa fedha za umma.
Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(kushoto) na Balozi wa Ujerumani nchini Klaus Peter Brandes (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano ya mkataba wa msaada wa miaka mitatu leo mjini Dar es salaam ambapo Ujerumani itaipatia Tanzania msaada wa Shilingi bilioni 352 . Msaada huo utasaidia kuboresha utawala bora katika serikali za mitaa, sekta ya afya , nishati , maliasili, maji, mfuko wa bajeti ya Serikali na kuboresha programu ya usimamizi wa fedha za umma.
Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(kushoto) akisoma hotuba mara baada ya kusaini hati ya makubaliano na Balozi wa Ujerumani nchini Klaus Peter Brandes (kulia) ya mkataba wa msaada wa miaka mitatu ambapo Ujerumani itaipatia Tanzania msaada wa Shilingi bilioni 352 . Msaada huo utasaidia kuboresha utawala bora katika serikali za mitaa, sekta ya afya , nishati , maliasili, maji, mfuko wa bajeti ya Serikali na kuboresha programu ya usimamizi wa fedha za umma. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar esalaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Mgimwa, hapa itapendeza kama tutachukua hizi bilioni 352 za msaada halafu tukatoa na kulipa bilioni 280 za mkopo wa juzi kutoka India, zikabaki bilioni 72 ambazo tutaweza kula bila hofu yoyote ile...

    ReplyDelete
  2. Hivi ni kwanini serikali huwa inapenda kusema ni misaada kwa wananchi na wakati si misaada? Hii ni mikopo na ina ambatanishwa na masharti makali.......huwa najiuliza siku zote, ni kwanini hata isisemwe tu ni mikopo?

    Kweli wananchi hawahitaji kujua hili? Wakati walipa madeni ni hao hao wananchi?

    ReplyDelete
  3. BILA SHAKA WATANZANIA TUNA LAANA. MIAKA HAMSINI YA UHURU, NA RASILIMALI ZOTE HIZI TULIZONAZO BADO TUNATEMBEZA MABAKULI UGHAIBUNI KAMA SUDANI KUSINI. AIBU KWA VIOGOZI WETU

    ReplyDelete
  4. Mara nyingi naona tunaambiwa tumepewa msaada na nchi fulani.
    labda niulize, hii misaada haina masharti?
    Ingependeza pia tukaambiwa tumepewa msaada wenye masharti au usio na masharti, au wenye masharti nafuu.
    ili walipa kodi tujue kabisa kama kuna deni litatukabili

    Ni mawazo yangu

    ReplyDelete
  5. Msidanganywe, hawa wazungu hawatoi msaada bila kupata kitu. Hapo wame-sign mikataba ya kupata Uranium, madini, kahawa kwa bei nafuu, na vingine vingi..hivi vitu bwana havina cha bure...kwani ninyi ni nani mpewe vitu bure? Mdau, USA

    ReplyDelete
  6. Hakuna nchi inayotoa pesa za bure. Nchi zote za majuu hukusanya kodi za mapato kutoka kwa wananchi wake. Nchi hizo si kwamba hawana kazi na pesa na kwamba waTZ ndio wanatakiwa watumie pesa zao. Hizi pesa zinakopeshwa tena kwa riba (interest) kubwa sana. Viongozi wetu hawajali mambo ya Riba kwani hiyo wanadhani haili kwao, bali inakula kwa wananchi walio wengi. Ni jambo la aibu sana kuona eti NCHI inakwenda kwa Bank ya Binafsi ya India kukopa pesa. Ni aibu kubwa!!!!! Na wao hawajali!!! maana wanatafuta pesa za uchaguzi sasa.

    ReplyDelete
  7. Aibu aibu aibu kwa nchi hii kuchukuwa misaada mpaka hii leo.

    ReplyDelete
  8. kama nilivyowahi kusema kwenye habari za juu kuwa tanzania tutabakia kuwa omba omba mpaka kwa wahindi ni aibu kubwa nchi inashindwa kusimama kiume mpaka leo hii

    mnatutia aibu kubwa sana watanzania kwa kugeuka omba omba fezeha kubwa sana serikali mnakomaa sana hamna hata aibu loooo shame on u.

    ReplyDelete
  9. Hizo hela zitaliwa vizuri na wajanja, hakuna cha maendeleo wala nini!! I still don't get it how these EEC countiries are still giving out money when they have serious problems in their countries. Not much jobs at all,some are basically struggling but they have money to dish out to corrupt countries like Tanzania.

    ReplyDelete
  10. hii inaitwa INZI STAYLE.

    ReplyDelete
  11. Mimi napendekeza serikali kukopa kwenye benki za ndani ili kuepuka risk ya interest rate, exchange rate cost na transaction cost, hivi vitu ndio ambavyo vinaongeza cost of debt kwenda juu zaidi ukizingatia kuwa Tanzania currency ni very weak kwahiyo haya madeni ambayo tunachukua kutoka hizi nchi za kigeni tutapata sana shida kuyalipa kwasababu hatuna control na pesa zinazotoka nje ni kujaribu kubalance economics kwa kuchukua mikopo zaidi ya ndani na ya nje iwe kidogo kwasababu ikiwa ni mikubwa tutakuwa tuna withdraw money kutoka kwenye uchumi wetu na mwisho wa siku uchumi hatakuwa unakuwa kama tunavyotaka.
    Mdau UK

    ReplyDelete
  12. hahaha mdau wa hapo juu u made my day eti HII INAITWA INZI STYLE yani tanzania ni sawa na inzi au paka la hotel

    ReplyDelete
  13. Jamani kwanini ?wananchi hatuambiwi ukweli? hivi hii ni misaada! kama ujerumani ni watoaji wa misaada mbona hawawapi misaada wenzao wa Ugiriki ? baadala yake wataka kuwakopesha,Serikali lazima hiwe makini sana na upokeaji wa hii mikopo,baadaye tutajikuta pa baya sana

    ReplyDelete
  14. Mhe.Mgimwa imenisikitisha sana kuona unasaini makubaliano huku bendera ya nchi imegeuzwa up-side down,hii maana yake nini?

    ReplyDelete
  15. pesa iliyorudishwa ya rada imeenda kununua madawati ya shule kila siku tunaona watu binafsi wanajitolea kununua madawati serikali ishakula pesa na hii pia wengine wanafungua account swiss hii leo ulaji kwenda mbele eti bongo inaendelea bongo inarudi nyuma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...