Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan (Bunge) Mhe. Hirotami Murakoshi kwenye chakula cha jioni Dodoma Hoteli. Waziri Murakoshi yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi.
Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashillilah (kulia) akiwakaribisha na kuwafunda waajiriwa wapya 19 walioajiriwa hivi karibuni katika ofisi ya Bunge.
Mhe. Azzan Zungu (kushoto), Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa Bunge akitoa ufafanuzi wa yaliyotokea siku alipotuhumiwa kutoa rushwa mjini Dodoma. Ameuhakikishia umma kwamba hilo si kweli.
Wajumbe wa Jukwaa la Katiba wakiwa na wanahabari mjini Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi jezi za michezo kwa timu ya Bunge chini ya nahodha wake Mhe. Idd Azzan, Mbunge wa Kinondoni Na Prosper Minja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Rushwa, rushwa na rushwa mbele kwa mbele! Rushwa yanukia kama harufu ya ubwabwa, tunaiskia na tunaambia ubwabwa haukupikwa bwana. Du! Nakumbuka hadithi za Abunuasi!

    ReplyDelete
  2. Siyo Rushwa inanukia tu, ipo na kama ni ubwabwa imepikwa kabisa watu wanaonja. Rushwa ni mchezo wa kawaida, kila wizara inatoa au inachukua rushwa. Siye na wa Nigeria sijui nani mkali kwenye ili, inasikitisha sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...