Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam jana, kuonesha hasira zao baada ya timu hiyo kusuasua katika michezo yake ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, ambayo ilifungwa bao 2-0 na Mtibwa Sugar, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Ujumbe kwa golikipa wa Simba, Juma Kaseja
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam jana, kuonesha hasira zao baada ya timu hiyo kusuasua katika michezo yake ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, ambayo ilifungwa bao 2-0 na Mtibwa Sugar, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nyie acheni kumkatisha tamaa kaseja, yaani kwa yepi hasa aloyafanya mpaka kuwakinisha hivyo? ni kwa hayo matokeo ya morogoro au kuna lingine?jamani tuwe na subira walau kidogo na lazima tuelewe kwamba hizi timu ambazo huwa zinafungwa mara kwa mara na haya matibu yetu makubwa nazo zinawashabiki vilevile na huwa wanaumia sana lakini huwa hawabebi bango wala kumsimanga mtu iweje leo nyie tu? ivi ni nyie pekee ndio wenye utashi na hisia za maumivu?

    ReplyDelete
  2. Pamoja na mapenzi na hasira za kufungwa ni lazima busara zitumike. Simba wamefungwa mechi moja tu tangu ligi kuanza, mbona Yanga na wengine wamefungwa zaidi na hawalaumu wachezaji? Kaseja kafanya makubwa sana ktk klabu, juzi alifungwa goli moja la makosa ila ndio sehemu ya mchezo, mbona wachezaji waliokosa magoli ya wazi na walinzi waliopitwa hawaguswi? Ninaweza kuelewa lawama kwa Kaburu maana anafanya kila kitu mwenyewe kama timu ni mali yake bila kusikiliza wadau. Yanga wamefanikiwa kwa sababu ya umoja na wanazidi kuongeza wadau wa kushirikiana nao, kwa Simba ni kinyume maamuzi yote anafanya Kaburu na wakati mwingine kuingilia benchi la ufundi, nadhani hilo ndio tatizo kubwa sana kwa Simba.

    ReplyDelete
  3. Mla akiliwa inakuwa hapatoshi!

    Hata Man unted yenyewe inafunga Timu nyingi sana lakini wakati mwingine nayo 'inaukalia' !!!

    Itakuwa ninyi Simba SC mmekuwa ni Man united msifungwe?

    ReplyDelete
  4. jamani,simba kushindwa mechi moja tu,Kaseja keshakuwa hafai?haifai hivo jamani!simba tushikamane.Kwangu mimi tatizo kubwa ni kule kutoka sare mara nyingi,hilo tulifanyie kazi!Nafikiri,Kaburu akae pembeni,amwachie mwenzake Hanspoppe akamilishe kazi.Ikimshinda lawama kwake.Hatuwezi kuwa na Marubani wawili wakishika Usukani mmoja kwa wakati mmoja,gari lazima litapinduka!Mimi nina imani na Hanspoppe,anao uwezo,na ndio kwanza kapewa hilo jukumu,na yeye atataka aonyeshe uwezo wake.Tumpe nafasi afanye vya kwake,lakini masikio yake yawe kwa wapenzi wa simba,wao ndio wanaoujua uwozo uko wapi!tulizeni boli,simba ushindi upo!

    ReplyDelete
  5. Acheni masihara Wana msimbazi anafungwa Spain Bingwa wa Dunia, anafungwa Real Madrid, anafungwa Bayern Munich, itakuwa ninyi?

    ReplyDelete
  6. Mtamkumbuka maximo. Lazima wabongo mjue si kila wakati mnafanya non-sense bali kufanya sense wakati wa kazi. Mzaha na upuuzi wa kaseja umetiponza na yeye huwa anajifanya nyerere kwenye timu.

    ReplyDelete
  7. Mlizoea Mipira ya Mipango Jijini Darisalama, ile kutoka tu nje ya nyumbani ,,,NGEDE!

    2-0 !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...