Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (katikati), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) alipokutana nao Wizarani jana. Mhe. Waziri alizungumza na Waandishi hao kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unotarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam tarehe 7 na 8 Desemba, 2012 na pia alijibu tuhuma kuhusu Meli za Iran kusajaliwa na kupeperusha Bendera ya Tanzania. Wengine katika picha ni Balozi Rajab Gamaha (kulia), Kaimu Katibu Mkuu na Balozi Dora Msechu, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Kimataifa
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifurahia jambo wakati wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe (hayupo pichani) alipozungumza nao.
Mhe. Membe akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani).
Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kutoka kushoto ni Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Irene Kasyanju, Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria.
Baadhi ya Watendaji wengine wa Wizara ya Mambo ya Nje waliohudhuria mkutano huo wa Mhe. Membe na Waandishi wa Habari. Kutoka kushoto ni Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw.Joachim Otaru, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango na Bw. Gabriel Mwero, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nilimsikiliza Membe jana kupitia Runinga(TV)moja,alipozungumzia kwamba kila nchi mwanachama wa SADC itaombwa isaidie chochote itakachoweza ili kufanikisha azma ya kurejesha utulivu na amani nchini Congo DRC,hususan katika maeneo ya Goma na North Kivu,na SANA,pale alipotamka wazi bila kubabaika kwamba,sisi Tanzania tutakuwa tayari kupeleka Batallion Moja ya Wanajeshi wetu,ili wakaugane na wenzao kutoka nchi zinginezo,ili kulinda amani,na kuiwezesha Cong DRC ipate muda wa kushughulikia matatizo yake ya maendeleo.That was very good,very inspiring!Tuliweza Afrika Kusini,vipi tushindwe Congo DRC?na wakati ule tulikuwa peke yetu au wachache sana,nchi nyingi zikitoa "lip service to the liberation of southern africa countries",lakini sasa tupo wengi,tuna marafiki wengi,vipi tuiachie Congo DRC itumbukie mikononi mwa Majasusi tena wasioitakia mema Afrika?Lazima tufike mahali,Umoja wa Mataifa tuombe msaada wa zana za "kivita" za ulinzi wa mipaka,na fedha kwa ajili kuendeshea harakati hizo,na wanajeshi wengi zaidi watoke katika nchi za SADC zenye machungu ya kutawaliwa,na zinazo tambua hatari za "nchi kuwa kibaraka",wachache sana waletwe na Umoja wa Mataifa.Congo DRC itatulia tu.Lakini,pia tusisahau kwamba,Congo DRC,ni nchi kubwa sana kiutawala,sawa na Western Europe yote,kwa hiyo,kazi ni kubwa!Lazima utazamwe uwezekano wa kuwepo kwa mfumo wa Utawala utakaowapa madaraka zaidi "wakazi wenyewe wa Kivu na Goma" waendeshe mambo yao wenyewe,lakini wakiwa chini ya Serikali ya Congo DRC(DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO,DRC)!hongera sana waziri membe kwa msimamo wako!tuko pamoja!ndugu zetu wa malawi wanasema,"Tiende Pamodzi!".Pamoja Tutashinda!Umoja ni Nguvu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...