Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza wakati wa maadhimisho ya  miaka 30 ya uzinduzi wa utiaji saini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Bahari ( UNCLOS) maadhimisho yaliyofanyika   Desemba 10 siku ambayo mwaka 1982 ndipo utiaji saini ulipoanza baada ya kuhitimishwa kwa mchakato wa majadiliano  magumu ya vuta nikivute yaliyodumu kwa miaka 10. 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Jaji  Joseph Sinde Warioba, Balozi Mstaafu Asterius Hyera na Jaji James Kateka ni miongoni mwa watu mashuhuri wanaokumbukwa kama chachu ya mafanikio ya kuanzishwa kwa mkataba huo ambao  katika duru za  Jumuiya ya Kimataifa unajulikana kama " Katiba ya Bahari" hadi sasa nchi 163 zimekwisha ama kuutambua mkataba huo au kuuridhia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mhe. Tuvako Manongi,

    Dondoo za Mkataba huo wa Bahari wa UN ndio za kuwatumia Malawi na Raisi wao Mama Joyce Banda wakae kwa amani na sisi Tanzania na waache madai yao ya kipuuzi kuhusu umiliki wa Ziwa Nyasa!

    ReplyDelete
  2. Mwanawane hivi Malawi wanahudhuria Mikutano hii kweli?

    Haya maazimio kama huu Mtakaba wa Sheria wa Bahari wanayaonaje huku wakilinganisha madai yao kuhusu Ziwa Nyasa?

    ReplyDelete
  3. Ama kweli !

    1.Unaweza ukasoma na usielimike!

    2.Unaweza kujua Kiingereza lakini usiyaelewe Masomo!

    Hivi Malawi wanawajumbe hapo Mkutanoni?

    Au Wajumbe wa Malawi wamelala kikaoni wakiuchapa usingizi huku maazimio yakipitishwa?

    Hayo Makubaliano ya Sheria ya Bahari halaingiliani na Sheria za Maziwa ya maji Duniani?

    Au Malawi watatoa hoja kwa Usomi wao watasema, ukilewa pombe ya ndizi au Gongo la Machungwa utakuwa umekunywa Juisi na sio Ulevi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...