Gwiji wa mashairi nchini HAMIS HIYANA almaarufu kama "Mkembebwenzi au Gendaheka" hatunaye tena. Marehemu Hamisi alifariki juzi (02.Desemba.2012) katika ajali ya gari iliyotokea Kibamba shule na amesafirishwa leo (04.Desemba.2012) kwenda kijijini kwao Mdaula, Bagamoyo. kwa mazishi.
Watanzania tunaungana na familia ya marehemu Hamisi Hiayana katika kipindi hiki cha kuomboleza msiba huu mkubwa wa mpendwa wetu.
"SISI SOTE NI WAJA, NA HAKIKA KWAKE TUTAREJEA".
|
Home
Unlabelled
mshairi gendaheka hatunaye tena
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mungu amlaze pema.
ReplyDeleteINNALILAH WAINA ILAYHI RAJIUN
ReplyDelete"INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUN"
ReplyDeleteMOLA pema akulaze, kwake umetangulia,
Nuruye akuangaze, lokosa kughufiria,
"Jannatu" akutembeze, milele humo bakia,
Hatunapo tujibanze, kifo yetu khatamia.
Mwenyeez Mungu akughufirie kwa yote na akupumzishe katika yake FIRDAUS - AMEN.
Inna Lillahi wa Ina Ilayhi Rajiuuuuuunnnnn !
ReplyDeleteRaha ya milele ampe EE Bwana, na Mwanga wa milele amuangazie, apumzike kwa Amani, Amen.
ReplyDeletePoleni wafiwa.
ReplyDeleteAjali zinatumaliza jamani japo zaweza kuepukwa. Tuziepuke kwa juhudi za mtu mmoja mmoja ama kwa juhudi za pamoja. Endesha taratibu. Ikibidi kulala sehemu, lala halafu kesho yake endelea. Kawia lakini ufike. Wasiwasi wangu huwa ni wale walevi wanao-overtake milimani, kwenye madaraja... Hawa wanaweza kukuua hata pale unapokuwa katika upande wako na ukiwa katika mwendo mdogo.
Serikali pia ina wajibu wa kutoa adhabu kali kwa ama wenye kuvunja sheria za barabarani ama wenye kusababisha vifo barabarani. Hii ya kulipa 20,000/= na kuondoka, si deterrant hata kidogo.
Tanzania ni nchi yangu lakini naogopa kuishi Tz. Sababu za kufa ni nyingi mno. Ukiweka pembeni stress za mgao wa umeme/giza, mfumo mbovu wa majitaka, kukatika kwa maji, rushwa sehemu za huduma, madereva wasio heshimu sheria barabarani, mishahara midogo nk nk. Kwa kweli hata kama una utajiri Tanzania, sioni unavyoufaidi katika mazingira haya.
Mdau wa Wed Dec 05, 11.23.00AM 2012,
ReplyDeletenakuunga mkono kwa asilimia mia moja, kuna mengi zaidi ya hayo uliyoyaorodhesha yanayonifanya nichelee kurejea TZ risk ni nyingi mno na maisha ya watu yanapotea kiurahisi mno kama wanyama inatia huzuni mno.