Kesho tarehe 7 Disemba 2012 kuanzia saa 3 asubuhi,rufaa ya kupinga ushindi wa Ubunge Jimbo la Ubungo,dhidi ya Mbunbe wa Jimbo hilo kupitia tiketi ya CHADEMA,John Mnyika itaanza kusikilizwa na jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufani. 

Mbunge wa Jimbo hilo la Ubungo,John Mnyika anawaomba wanachana na wampenzi wa chama hicho kufika Mahakamani hapo kwa wingi ili kusikiliza Rufaa hiyo,Kama alivyonukuliwa akisema "tulivyotafuta kura tulikuwa pamoja, tukapanga mstari kupiga kura pamoja na tukakesha kuzilinda pamoja tujumuike pamoja kujua hatma ya kura zetu".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. ndugu yangu Mnyika acha kupiga siasa kila mahali...hivi kweli unataka mimi nifunge duka langu hiyo kesho ili nije tu kukuangalia hapo mahakamani??Je hela ya kula kesho utanipa wewe kutoka kwenye mshahara wako mnono wa ubunge? Je kuwepo kwangu mahakamani kutabadilisha matokeo ya majaji??

    Ifike mahali wanasiasa wetu muwe mnatufikiria wananchi wenu tunavyoteseka na maisha na hata huo muda kidogo wa kupoteza ni gharama sana kwetu jamani.

    Jose - Kimara mwisho

    ReplyDelete
  2. Jose,

    Sisi hapa Kimara mwisho tutafika kwa wingi kesho, tulikuwa na kikao hapa kijiweni.

    Hivi kwanini wanamsumbua mbunge wetu kwa kesi za mara kwa mara?

    Mushi

    ReplyDelete
  3. Nilipoteza muda kupanga foleni kupiga kura yangu, lazima kesho niende kujua hatma yake.

    Hawa CCM waliokata rufaa wanatupotezea muda

    ReplyDelete
  4. Duh Hakika siasa ni inshu.... Bw Jose acha hizooo. W ewe kama hutaenda eti hiyo duka yako itafungwa basi baki siye tutakwenda!Hiyo shuhuli gani One man show!! Sasa uk*+a ndiyo basi tena!!

    ReplyDelete
  5. Wewe Jose huna lolote, hata kama uchaguzi utarudiwa wa kuitoa CHADEMA Ubungo hajazaliwa! hata wakiweka JIWE litashinda TU!

    Na huu ndio ukweli wa Jimbo la Ubungo! chezea wana Ubungo weye? wana msimamo kama SIMBA dume

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...