Kipa Bara, Juma Kaseja (kushoto) akiokoa moja ya hatari mbele ya mshambuliaji wa Zanzibar, Khamisi Mcha ‘Vialli’ katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole Kampala leo. Zanzibar ilishinda kwa penalti 6-5, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120, Bara wakitangulia kupata bao kupitia kwa Mwinyi Kazimoto dakika ya 10 kabla ya Abdallah Othman Ali kuisawazishia Zanzibar dakika ya 85. Mabingwa watetezi Uganda wameibanjua Kenya na kulinda ubingwa wao, wakiiachia Kenya nafasi ya pili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. well done ZANZIBAR huu mwanzo tuu heshma yetu na ya nchi yetu itarudi tuu kwa uwezo wa M/Mungu. well done and GOD BLESS ZANZIBAR.

    ReplyDelete
  2. Nchi yenu iko wapi? uko mbali na topic.

    ReplyDelete
  3. Tuachane na Zaznibar,

    Ankali kwenye mabishano na majadiliano ya Umoja wa Sarafu anayotoa Ndg. John Mashaka pana Mkenya mmoja anaitwa NAIROBIAN hivyo ni kuwa Matokeo ya CECAFA yanasomeka hivi:

    BAO LA MATOKEO BAADA YA FAINALI ZA CECAFA JIJINI KAMPALA-UAGNADA:

    NCHI/TIMU MABAO KTK MABANO
    1.TANZANIA (10)
    Kili Stars
    (Mdau wa Bongo No.13 aliyetoa pointi 10 za hoja ktk mabishano dhidi ya Mkenya-Nairobian)

    2.KENYA (0)
    Harambee Stars
    (Nairobiana)

    Hivyo Mshindi sio The Cranes Uganda ni Kili Stars kwa Mujibu wa Mabishano na sio Mpira ambapo Mkenya (NAIROBIAN) amepigwa Mabao 10 kwa 0 ktk Mechi ya Fainali!

    Mtanzania ametwaa Kombe kwa Ubishi!

    ReplyDelete
  4. Mpinga Muungano anony Sun Dec 09, 01:19:00 AM 2012

    well done ZANZIBAR huu mwanzo tuu heshima yetu na ya nchi yetu itarudi......and GOD BLESS ZANZIBAR

    Kwa taarifa yako Mwenyezi Mungu anachukia utengano unaoutaka wewe kwa kuukataa MUUNGANO!

    ReplyDelete
  5. Mdau wa kwanza wa ZANZIBAR unaota nini?

    Wenzio akina Seif Shariff Hamad, Hamad Rashid na KUNDI LA UAMSHO wanaimarisha Muungano wewe unaukataa?

    ReplyDelete
  6. Mpinga Muungano Mdau wa kwanza Sun Dec 09, 01:19:00 AM 2012

    ...Neema za Muungano utaziona pale unapopanda Boti kuja Bara ili kufuata vitu hivi:

    1.Konyagi-B (Gongo) wengi Waheishimiwa Visiwani mnakunywa lakini kwa siri lakini mkija Bara mnalewa bila woga kabisa!

    2.Miongoni mwenu wapo wanao muenzi Bob Marley na Siasa zake, huko mnavutia vyooni na mashambani kwenye minazi au pwani vichakani lakini Bara mnakaa Maskani mnastarehe!

    3.Usiku mnapata starehe kwa madada wa usiku bila woga wa Sheria kali zozote, lakini huko Kisiwani madada wapo lakini wanajificha!

    Sasa kwa neema adimu huko Zenji hizo (3) pekee hapo juu utasema Muungano haufai?

    ReplyDelete
  7. Mkataa Muungano wa kwanza Sun Dec 09, 01:19:00 AM 2012

    ...Wewe unatakiwa uje Bara ukitokea Zanji halafu ukute mimi Maganga wa Bara nimevaa msuli wangu kiunoni na flana lainiii halafu dada yako ananipikia chai kwa chapati na mchuzi wa samaki ndio utauheshimu Muungano!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...