Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakichangayika na wanakijiji wenzao wa kijijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani,kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za utamaduni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakichangayika na wanakijiji wenzao wa kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za utamaduni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kaka yake Mzee Selemani Kikwete kwa wanakijiji wenzake wa kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za utamaduni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa heri na wanakijiji wenzao wa kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, wakati wa kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za kienyeji.
Wanakiji wa Msoga wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani wakiangalia fashifashi wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kijijini hapo. PICHA NA IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. NNACHOKUPENDEA RAIS WANGU UNAJICHANGANYA KOKOTE TATIZO UNAOFANYA NAO KAZI NDO WANAKUHARIBIA... KILA LA KHERI

    ReplyDelete
  2. I agree with u above, the problem is the other Ministers and government officials. This guy a true Tanzanian, hawezi kuwa kila mahali na hawezi kuongoza kila wizara. We need a few January Makamba to assist him. At the moment, I doubt if we will ever get any maana wasaidizi wake wanakuula nchi utafikiri hakuna kesho!!

    ReplyDelete
  3. HONGERA RAIS UTAPOSTAAFU TUTAKUKUMBUKA SASA MAANA MARAIS WACHACHE HADI KUFANYA SHEREHE KIJIJINI DUUUU MUNGU AKUONGEZEE BARAKA

    ReplyDelete
  4. Watanzania bwana tunapenda kudeka, ni jukumu la kila Rais kuwa karibu na watu wake na si kufanya maigizo. Kwani hao wasaidizi wanaomuangusha hawaoni, hawasikii? Sote tuwajibike kwa bidii kama kweli tunataka Rais wetu awajibike ipasavyo kwetu badala kupiga picha na kula pilau nae kwani hizo si changamoto zinazotukabili kwa sasa.

    ReplyDelete
  5. Back to basics

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...