Picture
Waandaaji  wa mashindano ya  mbio za Kilimanjaro Marathon 2013 wametangaza kwamba mbio za mwaka huu zitafanyika katika njia zile zile zilizotumika mwaka jana. Mbio hizo limepangwa kufanyika Machi 3, mwaka huu mjini Moshi.

John Addison, Mkurugenzi Mtendaji wa Wild Frontiers, ambao ni waandaaji wa tukio hilo alisema katika taarifa jana kwamba njia zitakazotumika kwa ajili ya Kilimanjaro Marathon2013 ni kuanzia Uwanja wa chuo cha Ushirika (MUCCoBS) kuelekea katikati ya mji, na kisha kufuata barabara kuu ya kwenda Dar es Salaam kwa takriban kilomita 8 hadi 9, baadaye watageuka na kurudi Moshi mjini kupitia katikati ya mji, na badaaye watapandisha mwinuko kidogo kuelekea Mweka, “wanariadha watafurahia zaidi sehemu hii kwasababu ina mandhari ya kuvutia na kutakuwa na washangiliaji wengi  kando ya barabara”.

Addison anasema, “sehemu ya kupandisha kuelekea Mweka inahitaji kupanda kwa taratibu lakini kwa sababu Mlima Kilimanjaro ni kivutio na uwepo wa wananchi wanaoshangilia muda unaenda haraka na kuwasaidia wakimbiaji kumaliza mapema”.

Alisema kuwa kituo cha cha Mweka ambapo ndipo wanaridha waatakapogeukia ili kurudi uwanja wa Ushirika inakuwa ni takribani kilometa 32 tangu kuanza mbio ndefu ya kilomita 42. Baada ya hapo kipande kilichobaki inakuwa ni mteremko kuelekea uwanjani mwisho wa mbio na njia nzima ni mteremko tu.

Aliongeza kuwa kwa wale watakaoshiriki nusu Marathon, mbio zitaanzia uwanja wa MUCCoBS ambapo pako tambarare na baadae watapandisha kwenye mwinuko kidogo kuelekea Mweka kama ilivyo zile mbio ndefu kabla ya kurudi umbali wa takriban km 10, kuelekea tena uwanjani.

Kutakuwa na meza za maji kama ilivyo kawaida na magari maalum ya kunyunyizia maji mithili ya mvua kando ya barabara huduma ambazo zimeandaliwa maalum kuwafanya wanariadha waendelee kuwa na nguvu wakati wote wa mbio hizo.

Kuhusu burudani, Addison alisema kuwa hali ya uwanjani itakua ya kusisimua kutokana na burudani kali kutoka bendi za muziki wa nyumbani zitakazokuwepo, chakula cha kutosha, nyama choma na vinywaji na bila kusahau mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run ambazo pia zinatarajiwa kuleta msisimko wa aina yake.

“Ili kuhakikisha usalama wa wakimbiaji, baadhi ya barabara zitakuwa zimefungwa, asubuhi siku ya mbio, lakini kutakuwepo na njia mbadala kuzunguka mji kwa ajili ya wakazi wa Moshi. Wakazi wa Moshi ambao wanatarajia kukimbia pamoja na wakimbiaji wengine watakaofika Moshi mapema wanaweza kuanza mazoezi katika njia hizo hili kupata uzoefu wa njia na kujiandaa vizuri kwa ajili ya mbio.”

Mbio hizo zinaratibiwa na Executive Solutions na kudhaminiwa na Kilimanjaro PremiumLager, huku wadhamini wengine wa tukio hilo ni pamoja na Vodacom Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (Nusu Marathon Walemavu), Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, New Arusha Hoteli, Kilimanjaro Water, FastJet na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...