Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga, Pascal Lesoinne (kushoto), akikabidhi mfano wa hati kwa mmoja wa wasambazaji wa saruji ya TPCC, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mwanza Huduma Co Ltd, Zully Manji baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa jumla wa wasambazaji bora wa saruji ya Twiga,  katika hafla ya Usiku wa Wasambazaji wa Twiga Cement jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Twiga, Ekwabi Majigo. Alipewa zawadi ya tani 40 za saruji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga, Pascal Lesoinne (kushoto), akikabidhi cheti cha shukrani kwa mmoja wa wasambazaji wa saruji ya TPCC, Bi. Chaba Mavura ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Samks Traders Ltd, katika hafla ya Usiku wa Wasambazaji wa Twiga Cement jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Twiga, Ekwabi Majigo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga, Pascal esoinne (kushoto), akikabidhi mfano wa hati kwa Mkurugenzi  wa kampuni ya V.G.K Ltd, Valence Msack kama uthibitisho wa zawadi ya tani 25 za saruji iliyopewa  kampuni hiyo baada ya kuibuka mshindi wa tatu wa wasambazaji bora wa saruji za Twiga, katika hafla ya Usiku wa Wasambazaji wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Twiga, Ekwabi Majigo
 Baadhi ya wasambazaji wa saruji ya Twiga na wafanyakazi wa TPCC wakiselebuka katika hafla hiyo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...