Mgombea nafasi ya Uwenyekiti wa ya Miundombinu  Mhe. Peter Serukamba ane akinadi sera zake mbele ya wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi leo
 Mgombea nafasi ya Uwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto Kabwe akinadi sera zake mbele ya wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi leo
 Mgombea wa Nafasi ya Uenyekiti katika kamati ya LAAC Mchungaji Israel Natse nae akinadi sera zake
 Wajumbe wa Kamati ya PAC wakiteta na Mhe. John Cheyo anaye tetea kiti chake cha uenyekiti wa kamati 
 Mhe. David Kafulila akimpongeza Mhe. James Lembeli mara baada ya kupita bila kupingwa kwa nafasi ya uenyekiti wa kamati ya Ardhi  Maliasili na Mazingira 
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akizungumza na wajumbe wa kamati ya Bajeti ambapo tofauti na kamati nyingine amefanya uteuzi wa mwenyekiti wa kamati hiyo kuwa Mhe. Andrew Chenge.
 Katibu wa Bunge Ndg. John Joel akitangaza Matokeo ya wenyeviti na Makamu wa Wenyeviti mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa viongozi hao katika kamati zote za Bunge leo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa kamati za Bunge Ndg. Theonist Luhirabake na kulia ni Afisa Habari wa Bunge Ndg. Owen Mwandumbya 
 Msimamizi wa Uchaguzi katika kamati ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa kimataifa Bi. Justina Shauri akiwapa maelezo ya awali wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuchagua viongozi wao.
 Msimamizi wa Uchaguzi katika kamati ya Ulinzi na Usalama Ndg. Peter Magati akiwapa maelezo ya awali wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuchagua viongozi wao. 
 Katibu wa Kamati ya PAC Bi. Lina Kitosi ambaye pia ndiye msimamizi wa uchaguzi akiteta jambo na mwenyekiti wa mda wa kamati hiyo kabla ya uchaguzi kufanyika.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...