Urban Pulse Creative inakuletea taswira kutoka Westminister Abbey jijini London katika misa maalum ya kuombea amani nchi yetu ya Tanzania siku ya muungano iliyofanyika ijumaa tarehe 26.4.13.

Balozi wetu Mh Peter Kallaghe, maofisa kutoka ubalozini na baadhi ya watanzania waishio nchini Uingereza walijumuika pamoja kuhudhuria ibada hii maalum na raia wengine kutoka nchi mbalimbali. Ibada ilianza kwa jumuiya ya Abbey kuwaombea watanzania wote, viongozi pamoja na wanadiplomasia wote waliopo duniani na kwa ajili ya kazi maalum ya Ubalozi wetu hapa nchini Uingereza.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA

Asanteni,

Urban Pulse Creative
Mh Balozi Kallaghe akisalimia na Kiongozi wa kanisa baada ya ibada.
Bendera yetu ikipepea.
Kanisa la Westminister Abbey London.
Kutoka kushoto Abu Faraji, Caroline Chipeta, Mirium Mungula na mdau baada ya ibada.
Wazee wa kazi.
Picha ya Pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ni westminister au westminster?

    ReplyDelete
  2. Mungu azidi kuibariki Tanzania na Watu wake. Amen.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2013

    Haha, na kweli tunahitaji kuombewa!!! Sala hizo zitamaliza ufisadi sugu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2013

    Maombi mengine ya ziada ya kumpelekea Mwenyezi ni sisi kupata ujasiri na uwezo wa kuwawajibisha Wahalifu!

    Mfano:

    1.Mafisadi
    2.Wala Rushwa
    3.Matapeli
    4.Wadukuzi wa wachochezi
    5.Vishoka ktk huduma za Jamii.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2013

    Mdau wa Kwanza umenikumbusha mambo ya:

    Kazimia=JOB HUNDRED

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...