Kamanda Mpinga unaiona hii ya leo karibu na New Msasani Club Barabara ya Mwai Kibaki Road jijini Dar es salaam? Huyo dereva sio tu aliamua kupita katikati ya foleni bali pia alikuwa katika mwendo wa kasi na fujo huku akipiga honi. Mie mwenyewe kanikosa kunipiga pasi Kitetenesi changu....Wanaomjua wanasema dereva huyo hizo ndio zake na hakuna wa kumgusa (ati hata wewe) kwa kuwa yuko 'Connected'. Je ni kweli jamaa yuko juu ya sheria??
Mdau Msasani Kwa Mwalimu
HEBU TUONGEE NA MAKAMANDA ILI KAMERA ZIANZE KUWA DILI YAANI TUANZISHE BLOGU LA USALAMA BARABARANI TU NA HAPO UKIPELEKA PICHA YA FAULO BARABARANI IKWA NI PAMOJA NA DALADALA KUPAKI NJE YA VITUO AKIKAMATWA NA KUPIGWA LIFAINI LAKE KAMA LAKI HIVI UNAPEWA ANGALAU 30,000/= TUONE KAMA HAWATAACHA!
ReplyDeleteWazo lako nzuri sana mdau wa kwanza, si wewe tu tena katika blog hiihii watu mbalimbali walishaleta mawazo kama hayo kwa matukio kama haya kwa upande wa mabasi yaendayo mikoani, nachelea kusema bongo mawazo yenye kujenga hawana haja nayo kaka,Walikuja watu wazuri wenye mawazo mazuri tena ya kizalendo leo wametuachia majonzi,wametutangulia,walishauri mengi yenye maslahi lakini walipuuzwa.
ReplyDeleteHiyo Costa ni ya mmoja wa Kamanda wa Polisi tena mkubwa nafikiri ni ya Mahita hizi
ReplyDeleteNini 30,000? Mpelekeni pale Sumatra ofisi ya Mwalimu haouse wale jamaaa ni noma! hawana salie mtume, walinisulubu sana na Noah yangu na huwezi kuwashawishi.Angekoma ndugu
ReplyDeleteHata Mimi nimewahi kukumbana na dala dala hii siyo mara moja. Dreva huyu anaendesha kama ndio yeye tu katika barabara. Inasikitisha sana.
ReplyDeleteDu jamani nilizani ni mie peke yangu mie nusu aniingize kwenye mtaro pale chama kisa basi la kigogo wa polisi, tafadhali tunaomba jeshi la polisi kikosi cha barabarani wamfuatilie dereva huyu mbona NANGA BOY mambasi ya mwenge posta mpaka kunduchi na yenyewe ni ya mzito ila angalia vijana wale walivyo na nidhamu barabarani.
ReplyDeleteMnapiga blah blah tuu... hata madereva wa magari mnatua hovyo hovyo... Kamanda Mpunga sio mwenye makosa; ameshatoa rai madereva wafuate sheria; ila mnakaidi hata huyu dereva(mwehu) anakaidi. Madereva mnatakiwa mjifikirie na kubadili tabia.
ReplyDelete