Gari iliyobeba mwili wa Marehemu Ayubu Mlay ukiwasili kijijini kwao Sango, Moshi tayari kwa mazishi leo
 Marafiki wakiwa wamebebe jeneza lenye mwili wa Marehemu Ayubu Mlay ulipowasili kijijini kwao Sango, Moshi tayari kwa mazishi leo
Nyumba ya milele ya ndugu yetu Ayubu Mlay kijijini kwao Sango, Moshi.
Marehemu, aliyekuwa mfanyabishara mashuhuri wa magari, aliuwawa kwa kupigwa risasi majuzi katika klabu ya Ambrosia Mbezi Kwa Zena-Kawawa jijini Dar es salaam. Picha zote na Kipepeo Tours
Kwa habari hizo kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2013

    Pamoja na kuanzishwa usajili wa slaha bado udhibiti na utoaji vibali vya kumiliki silaha umekuwa ni mdogo sana siku hizi, vijana wengi ambao uadilifu wao ni wa kutilia mashaka wanamiliki silaha na kuziweka hadharani kwa mbwembwe bila woga na wengine wanaripotiwa polisi bila hatua kuchukuliwa. Mauaji ya kijana huyu ni moja ya matukio niliyoongelea hapo juu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2013

    Tusipoangalia yatatufikia yale yaliyowapata wamarekani hasa weusi juu ya umiliki wa silaha holelela na kuishia kuundwa kwa gangs na kuuwana wenyewe kwa wenyewe.

    ReplyDelete
  3. Msema kweliMay 24, 2013

    Tena muuaji ni mtu wa vitisho kwa wenzie sana na polisi wanajua hilo kwani sio mara moja au mbili taarifa kutolewa polisi lakini ktk mazingira 'yale ya polisi' huwa anarudishiwa silaha hiyo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2013

    Mdau wa May 24, 2013.
    Jamani kama ishu huijui afadhali kukaa kimya wa kwetu, au omba uelemishwe. Unasema "Tusipoangalia yatatufikia yale yaliyowapata wamarekani hasa weusi juu ya umiliki wa silaha holelela na kuishia kuundwa kwa gangs na kuuwana wenyewe kwa wenyewe." Je unajua nani anatengeneza hizo silaha? Jibu ni rahisi. Sasa wewe unawalaumu weusi kwa kuuana, wanapata wapi hizo bunduki?!! Kwanza ni makosa kwa kufafanisha Bongo na Marekani-yaani huu mjadala hauendani. Bongo tuache kabisa kujifanya tuko sawa, au mambo yetu ni kama Marekani. Tunatia aibu napoona watu wanaropoka ovyo. Naishia hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...