JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI        
  
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
30/05/2013

Baadhi ya vyombo vya Habari vimekuwa vikitoa taarifa potofu kwamba kumekuwepo na upotevu wa shilingi 252,975,000,000.00 ambazo zimelipwa kwa miradi hewa.  Wizara inapenda kutoa taarifa rasmi kwamba taarifa za vyombo hivyo vya habari si za kweli na zinalenga kupotosha umma. 
Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) inatekeleza miradi mingi ya barabara nchini.  Hivi sasa miradi ya barabara yenye urefu wa Km. 11,154 ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji kote nchini. 
Ujenzi wa Barabara hizi hutumia fedha nyingi na Serikali inalipia kazi hizo za ujenzi kulingana na hati za madai (Interim Payment Certificates – IPCs) zinazotoka kwa Wakandarasi na Wahandisi Washauri wanaojenga na kusimamia miradi hii.  Aidha, malipo hufanyika baada ya IPCs kuhakikiwa na Wahandisi Washauri, TANROADS na Wizara yenyewe. 
Ili kufanikisha azma ya Serikali ya kuimarisha mtandao wa barabara nchini, katika mwaka wa fedha 2011/12 Serikali iliweka Kasma maalum ya ujenzi wa miradi ya barabara na kuitengea jumla ya shilingi 252,975,000,000.00 katika bajeti kwa ajili ya kulipia kazi za barabara zinazoendelea. 
Fedha zote zilitolewa na HAZINA kwa madhumuni hayo na kwa kufuata taratibu za Serikali.  Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS ililipia kazi za barabara kwa maana ya madai ya Wakandarasi na Wahandisi Washauri wa miradi mbalimbali inayoendelea.  Aidha, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alipatiwa na anayo taarifa ya jinsi fedha hizo zilivyotumika. 
Fedha hizi zilitumika vizuri na zimesaidia kufanikisha utekelezaji wa programmu ya barabara nchini kwa kulipia madai ya Wakandarasi na Wahandisi Washauri kwa wakati.  Aidha, katika Mwaka 2011/12, Wizara ilitumia zaidi ya shilingi 252,975,000,000.00 zilizotengwa kupitia mradi maalum.  Kazi za barabara kwa jumla zilitumia  shilingi 662,308,000,000.00 fedha za ndani. 
Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa ufafanuzi huu na kuudhibitishia umma kuwa hakuna upotevu wowote wa fedha. Taarifa zinazotolewa katika  baadhi ya vyombo vya habari kuwa kuna upotevu wa fedha ni za upotoshaji.

Balozi Herbert E. Mrango
KATIBU MKUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...