Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Uholanzi (NUFFIC) Bwana Freddy Weima aliye kushoto kwa Balozi Kamala. Mwanzo kulia ni Bi Ute Jansen Mkuu wa Kitengo cha Mpango wa Uholanzi wa Kujenga Uwezo wa Vyuo Vikuu(NICHE) na wa pili kulia ni Bi Johanna Van Nieuwenhuizen Mkuu wa Idara ya Utawala ya NUFFIC. Balozi Kamala ameishukuru Uholanzi kwa kubuni na kutekeleza mpango wa kusomesha Watanzania Uholanzi kupitia taasisi ya NUFFIC na ameomba Uholanzi kuendelea kutekeleza mpango huo. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya NUFFIC amebainisha kwamba Serikali ya Uholanzi imeongeza miaka minne kuanzia tarehe moja mwezi ujao kuendelea kusomesha Watanzania Uholanzi katika vyuo mbalimbali. Balozi Kamala ameishukuru serikali ya Uholanzi kwa uamuzi huo. Balozi Kamala amekutana na viongozi wa taasisi ya NUFFIC leo hii ofisini kwao, The Hague, Uholanzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2013

    Wanaosomeshwa kwa misaada ya serikali hawana faida yoyote kwenye nchi yetu.Wakimaliza masomo yao huko nje wanakuja kugombania ubunge na kujinufaisha wao tu.Hakuna mwenye uchungu na nchi.
    Tunataka wasomi watakaojenga nchi yetu kwa moyo mmoja.
    Ni viongozi wangapi wanauchungu na maendeleo ya nchi?
    Kwani hao wanaotoa misaada walianzia wapi?
    Wakati umefika wa kusaidia jamii ya watanzania na sio kujilimbikizia mali kwa kutumia madaraka uliyopewa na wananchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...