Wahabeshi 18 na raia mmoja wa Kenya wakiwa makao makuu ya idara ya Uhamiaji mkoani Tanga ambapo walikuwa wakiandaliwa mashitaka kabla ya kufikishwa mahakamani Jumanne wiki hii kwa kuingia nchini bila kibali. Picha na Mashaka Mhando, Tanga

Na Mashaka Mhando,Tanga

IDARA ya Uhamiaji mkoani Tanga, inawashikiliwa raia 18 kutoka Ethiopia na raia mmoja wa Kenya, kwa kuingia nchini bila kibali.

Ofisa Uhamiaji wa mkoa wa Tanga, Bw. Sixtus Nyaki, alisema ofisini kwake kwamba raia hao, walikamtwa Juni 9 mwaka huu, kwenye nyumba moja eneo la Sahare katika Jiji la Tanga.

Alisema idara yake ilipata taarifa kwamba kuna nyumba moja ya Mtanzania mwenye asili ya Pemba, alikuwa amewahifadhi watu wengi kwenye chumba kimoja na hivyo maofisa Uhamiaji wakiongozana na askari polisi, waliwakuta wakiwa wamejibana kwenye chumba hicho kilichokuwa na kitanda kimoja.

Hata hivyo, Ofisa huyo hakuwa na maelezo zaidi kuhusu watu hao ambao hawajui kuzungumza Kiingereza zaidi ya Kihabeshi, hawajapata taarifa kujua wametumia usafiri gani kufika hapa nchini na wanaendelea na uchunguzi kujua hali hiyo.

Inaaminika kwamba Wahabeshi hao wametumia usafiri wa majahazi kutokea Mombasa nchini Kenya na wamehifadhiwa hapo ili waweze kutafutiwa usafiri mwingine kwenda Afrika Kusini ambako huko wamekuwa wakitafuta nafasi za kwenda nchi za Ulaya na Amerika.

Wimbi la Wahabeshi kuingia nchini hasa kupitia katika mkoa huu wa Tanga limeshika kasi zaidi kutokana na kuelezwa kwamba raia wamekuwa wakipita kutokea nchini Kenya kwenda Afrika Kusini kutafuita maisha.

Mwishoni mwa wiki Wahabeshi wengine wapatao 26, walimaliza vifungo vyao vya miezi mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kuingia nchini bila vibali na idara hiyo iliwasafirisha kurudi makwao.

Wahabeshi hao walikamatwa katika eneo la kizuizi cha polisi Kabuku, wakiwa wamepakiwa kwenye kontena la lori hivyo wakati wakipita hapo polisi walisikia sauti za watu wakitaka kutoka ambapo walipolifungua waliwakuta Wahabeshi hao ambapo wengine sita walikutwa wamekufa kwa kukosa hewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...