HABARI ZIMETUFIKIA PUNDE TU ZINASEMA MFANYABIASHARA MMOJA MAARUFU NCHINI SAID MOHAMED AMEMWAGIWA  KITU KINACHODHANIWA NI TINDIKALI NA WATU WASIOJULIKANA MAENEO YA MSASANI JIRANI NA KITUO CHA POLISI CHA OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM.

MFANYABIASHARA HUYO ANAEMILIKI MADUKA YA HOME SHOPPING CENTRE INASEMEKANA AMEPATWA NA SHAMBULIO HILO MARA BAADA YA MUDA WA KUFUTURU.

AIDHA, WANAHABARI WETU WAMESHUHUDIA MAGARI KADHAA YA POLISI YAKIWA KWENYE MAEGESHO YA DUKA MOJA KUBWA  LILILOPO MAENEO KARIBU NA OYSTERBAY POLICE, AMBAKO HAKUNA ALIYETAKA KUSEMA CHOCHOTE, JAPO HABARI ZINASEMA HAPO NDIPO TUKIO LILIPOTOKEA.

JUHUDI ZA KUMSAKA KAMANDA WA POLISI MKOA WA KINONDONI AMA KAMANDA WA KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM AFANDE SULEIMAN KOVA ZINAENDELEA. NASI TUTAWAJULISHA KILA TUTAPOPATA HABARI ZAIDI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2013

    mbona unajinyea kumtaja huyo mhusika kuwa ni said nanihii yule kijana mfupi wa kiarabu mwenye maduka ya nanihii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...