Na Mwandishi Wetu Dodoma

MPANGO wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora umeshauri kuwa ili kuboresha mazao ya kilimo na vyema sera na mikakati inayoendelea kutekelezwa na Serikali ikalenga zaidi kuwafikia wananchi walio wengi.

Hayo yamesemwa mjini hapa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa APRM Tanzania, Bw. Hassan Abbas alipokuwa akizungumza kuhuru matokeo ya utafiti wa APRM kuhusu masuala mbalimbali ya utawala bora nchini.

“Ripoti ya APRM pamoja na kuangalia masuala mengine ya siasa na utawala bora pia imeangalia namna nchi yetu inavyotekeleza sera na mikakati mbalimbali ya kukuza maisha ya watanzania ikiwemo kilimo.

“Ripoti ya APRM inayo mapendekezo yanayogusa sekta ya kilimo hususani umuhimu wa kuboreshwa sera na uwekezaji katika kilimo ili kukuza uzalishaji wa mazao lakini pia kuwawezesha wakulima kujinasua kutoka lindi la umaskini,” alisema katika Banda la Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Wakulima, Nane Nane yanayoendelea mjini hapa.

Bw. Abbas alisema Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zilizopiga hatua katika kuweka mikakati ya kuboresha kilimo na akasem a Ripoti ya wataalamu wa APRM imeguswa na Mkakati wa Serikali wa Kilimo Kwanza kuwa ni hatua nzuri ya kufikia mapinduzi ya kilimo.

Hata hivyo alionya kuwa kwa mujibu wa misingi ya utawala bora ni vyema sera na mikakati iliyopo vikatekelezwa kwa kuwshirikisha wakulima na wadau wengine ipasavyo.

“Kwa kuwa moja ya malengo ya Mpango wa APRM Afrika nzima ni kueneza dhana ya utawala bora hasa utawala shirikishi, nasi tunatumia fursa hii ya Maonesho ya Nane Nane kusisitizia kuwa kilimo chetu kitapiga hatua iwapo wananchi watashirikishwa katika kila mikakati na pia wakipewa fursa ya kutoa mrejesho wa sera na mikakati hiyo kwa nia ya kuboresha,” alisema.

 APRM ni Mpango wa viongozi wa Afrika ulioanzishwa mwaka 2003 kwa lengo la kuhakikisha kuwa nchi za Afrika zinawashirikisha wananchi wao katika kubaini na kuzitatua changamoto za kiutawala bora.

Bw. Abbas alisema kuwa Tanzania ilijiunga na Mpango huo mwaka 2004 na imekuwa ikitekeleza hatua za Mpango huo kiufanisi. Alisema kuwa Ripoti ya APRM inayoainisha masuala mbalimbali nchini itazinduliwa Oktoba mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...