Mmoja wa watoto wanaendelea na matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akiwa bize na rangi wakati walipotembelewa na mchora katuni Nathan Mpangala kupitia mradi wake wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Jumamosi iliyopita. Mradi huo unaoshirikisha ndugu, jamaa, marafiki na wachoraji wenzake, ulikwenda kuwafariji kwa kuwapa zawadi kisha kuchora nao.
Mratibu wa mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Katunisti Nathan Mpangala ‘Mtukwao’, akishea jambo na mmoja wa malaika Hospitali ya Taifa Muhimbili, upande wa saratani, Jumammosi iliyopita.
Marafiki wa Wafanye Watabasamu, walionesha tabasamu mapemaaaaa.
Sanaa inamchango mkubwa katika kupunguza msongo wa mawazo na kusahaulisha maumivu.
Mchora vibonzo wa ITV ambaye pia ni mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala akiwa na mchora vibonzo wa baadae.
NYUMBA TU, SIMPO. Akiendelezwa atakuja kuwa mchoraji mahiri wa majengo.
Mchoraji katuni wa gazeti la Nipashe, Abdul King O aka ‘Kaboka mchizi’, aliungana na Wafanye Watabasamu kuwatabasamisha malaika hawa.
Mungu akubariki Nathan na wote mlioshiriki.
ReplyDeleteNathan, ndugu na marafiki zako Mungu awabariki kwa kazi nzuri ya kujitolea. Big up sana sana
ReplyDeleteAbdul King O,tuttafutane bhana japo kwa salaam tumepoteana sana
ReplyDeleteBard Mkoba wa mchikichini
0655566555
Good work Nathan Mpangala, I am impressed with this.
ReplyDeleteMungu awazidishie Nathan na wote mlioshiriki kuwatembelea malaika hawa.
ReplyDeleteHivi mafisadi yenye mabillions hayana hata aibu, hizo hela walizotuibia zingekuwa zinawsaidia hawa watoto.
ReplyDelete"Artist must be true" Nathan you proved it. mungu akuzidishie na akupe ubunifu zaidi wa kuifanya jamii yako iendelee kutabasamu
ReplyDelete