Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Kisarawe hivi karibuni wakati alipowasili katika Shule ya Sekondari Msimbu iliyopo wilaya hiyo mkoani Pwani ili kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi.Fatuma Kimario .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msimbu iliyopo wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani wakati alipowatembelea hivi karibuni. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya kisarawe Fatuma Kimario,na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri Adam Ng’imba anayefuatiwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Zipporah Simwanza.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) akizungumza hivi karibuni na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msimbu iliyopo wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani juu ya umuhimu wa elimu na athari za mimba za utotoni wakati alipowatembelea wanafunzi hao.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi.Fatuma Kimario akisisitiza jambo wakati Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipotembelea Shule ya Sekondari Msimbu na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo ambapo aliwaasa wapende shule na kuepukana na mambo mabaya kama vile mafataki na uvutaji bangi ili waweze kufikia malengo waliojiwekea,kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) anayefuatia ni Mwenyekiti wa Halmashauri Adam Ng’imba na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Kisarawe Bi.Tatu Kano.Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...