Mkutano wa pili wa kimataifa wa masuala ya uendelezaji wa nishati ya  mafuta na gesi ulimalizika alhamisi jijini Dar es salaam Tanzania ambapo ulijumuisha serikali, taasisi za umma na makampuni mbali mbali.

Mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi nchini Tanzania (TPSF)  Dkt. Reginald Mengi ambaye alikuwa ni mmoja wa watoa mada akizungumza na Sauti ya Amerika kuhusu pendekezo lake la kusitishwa ugawaji wa vitalu amesema hilo halikufanikiwa kwasababu kinachompa shida ni kwamba hakuna sera ya kugawa au kutoa vitalu.

Aliongeza kuwa wakati huo huo  vitalu hivyo vinatolewa kwa wawekezaji wa kigeni, alihoji  katika mkutano huo kuwa inakuwaje wagawe rasilimali za taifa bila sera maana ukifanya hivyo ni  uporaji tu. 

Alisisitiza  kwamba mtanzania hafaidiki  na hajaona chochote  cha kusema kwamba mtanzania atawezeshwa  kwasababu sheria ya mwaka 2004 inasema wazi wazi kwamba watanzania watawezeshwa kumiliki uchumi wao.

Kuhusu  mazungumzo yake na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Bw. Eliakimu Maswi  amesema hakukuwa na makubaliano ya aina yeyote ni mazungumzo tu , na tunapoendelea kuzungumza vitalu vinauzwa , kwahiyo haoni kama kuna nia njema kushirikisha wazawa wa Tanzania katika sekta ya gesi hasa katika ugawaji wa  vitalu.

Kutokana na kauli iliyotolewa na waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo amemshauri arudi darasani akafundishe kwasababu anavyofikiria watanzania siyo wanafunzi wake darasani akiongeza kuwa mawazo yake hayana tija kwa wizara anayoongoza na wafanyabiashara wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Dkt.Mengi waziri huyo alikaririwa na vyombo vya habari nchini humo akisema kuwa wafanyabiashara wa kitanzania wanajua  biashara ya kuuza juisi tu jambo ambalo alisema ni tusi.

 Mkutano huo ulifanyika kutokana na  hatua ya hivi karibuni ya kugundulika kwa mafuta na gesi  nchini Tanzania. Waziri Muhongo akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni alisema hakuna Mtanzania mmoja mmoja atakayemiliki kitalu ila watanzania watawakilishwa na TPDC.Kusikiliza mahojiano hayo ungana na idhaa ya kiswahili ya sauti ya Amerika. http://www.voaswahili.com/content/article/1776533.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ubinafsi unatugharimu watz! Watu wanatumia taasisii fulani kutaka kujinufaisha na familia zao. Waziri muhongo endelea na kazi wazalendo tuko nyuma yako, tpdf ifanye kazi kwa niaba yetu.

    ReplyDelete
  2. Tuko nyuma ya Muhongo. Pato la TPDC ni la watanzania wote. Pato la hao walafi/wabinafsi na wapiga makelele ni lao na familia yao. Gesi ibaki mali ya umma kwa faida ya umma.

    ReplyDelete
  3. La kwanza sijui ni kwa nini mh Mengi alitutangazia mara ya kwanza kuwa wameridhika.

    pili mi binafsi nashindwa kujua yupi ni yupi na mkweli ni nani kwa sababu serikali ina rcord ya kuvurunda kwenye maswala ya mali zetu na pia serikali ijitathmini kuhusu sera iliyopigiwa kelele na Zitto sasa na Mengi kwani huwa baadae ndo watanzania tunajua kuwa kuna madudu.

    Na serikali ijaribu kuwaamini na kuwawezesha watanzania badara ya kuwakashfu hii itasaidia kwani sijui hata hao wanaokuja hawakuwa na hiyo mitaji walianza kama sisi.

    ReplyDelete
  4. Mengi asianze malalamishi yake yale yale ya Kilimanjaro Hotel aliyotaka kupiga rangi tu na kuifanya mgahawa! Leo tunayo hotel ya daraja la kwanza pale. Hawa wazawa tuwasaidie lakini tujue ukoo wao. Sheria yetu ilazimishe ubia na wazawa kwa asilimia inayoeleweka na kwa uwezo unaofahamika. Leo mengi na gesi wapi? Hii sio gesi ya coca cola! Muhongo oyee!

    ReplyDelete
  5. Hope tpdc kutakuwa hamna wala rushwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...