TAHADHARI:- KUNA TAPELI MWENYE ASILI YA KIZUNGU ANADAI YEYE NI RAIA WA AFRICA KUSINI. Ni  MREFU, ANAONEKANA SANA MITAA YA KINONDONI KWA MANYANYA JIJINI DAR MIDA YA USIKU. AMETAPELI WATU WENGI SANA AKIDAI KUA AMEIBIWA HOTELINI NA MWANAMKE NA ANADAI ANAISHI MBEZI KIMARA. KWA WENYEJI WENGI WA KINONDONI WANAMFAHAMU NA WENGI WAMESHAMSIKIA NA WANADAI NI MSWAHILI. CHUKUENI TAHADHARI NA TUKO KWENYE HARAKATI ZA KUMKAMATA KWA SABABU AMESHA TAPELI WENGI AKIJIFANYA KUCHUKUA NAMBA ZA SIMU KWA AJILI YA KUREJESHA FEDHA HIZO TUNAOMBA WENYE TARIFAA ZAIDI WATUSAIDIE KWA USHIRIKIANO NA POLISI KUMTIA MBARONI IMETOLEWA NA MMOJA YA WALIOLIZWA  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. TIT FOR TAT...No Complain please, Mmewaliza sana wathungu, Nao sasa zamu yao! ahahaha... This is Africa Bwana. kuna vihoja hadi Raha, Naipenda Afrika. Yani am so happy nilizaliwa mwafrika. poleni mliopigwa na mthungu, hehehe Bongoooo!!Safi sana. Tafuteni ule mwimbo wa Professor Jay, Bongo Dali salamu. Aliyaona haya akayaimba. LOLZ

    ReplyDelete
  2. Hakuna Mzungu aliyekuwa sio tapeli. Hata kama ni Profesa. Jihadhari na Wazungu. Mzungu yeyote anaishi kwa leo. Atafanya chochote ili afikie lengo hilo. Kama kutapeli kutamfanya aishi basi atatapeli.

    Mdau
    UK

    ReplyDelete
  3. Weee huo ndio ujinga wetu, sasa unampatia pesa mtu ambaye humjui au kwa vile Mzungu!! Ajabu, wala huna haja ya kutangaza acha azitafune hizo pesa hamna kazi nazo

    ReplyDelete
  4. Huyo Tapeli amekuwepo muda mrefu (ama mzungu mwingine tapeli kama siyo yeye). Alikwishaniliza Mikocheni. Alijitambulisha kuwa American japo accent si American. Nilimwamini kwa vile si Waamerika wote wana American accent. Anaomba pesa kuwa ameibiwa na amekwama hotelini. Anatembea sana kwa mguu. Na anakuwa ametoka jasho sana. Lakini kwa vile anaomba watu wengi kwa siku huwa hawakumbuki sura anazoomba. Baada ya kunitapeli Mikocheni, siku nyingine akanisimamisha mjini na story ile ile. Nikamwambia kuwa nilikwishamsaidia huko nyuma kwa hadithi hiyo hiyo. Akaona aibu akaondoka. Lakini kabla ya hapo nilikuwa nimekwishamwona kwa mbali akisimamisha watu wengine pia na kuwatapeli. Siku moja akanisimamisha tena Kijitonyama na kutoa hadithi hiyo hiyo. Siku hiyo nikamuitia polisi (CID) kwa simu. Polisi alipokuja akaongea nae halafu akamwachia. Kwa hiyo polisi hakuna msaada juu ya hili. Ni wananchi wenyewe tu wajihadhari.

    ReplyDelete

  5. we mpuuzi hapo juu kwani na walio walipo tugeuza slaves na kutufanya kama properties unadhani ilikua haki?? tena waacha wazidi kulizwa huyo mzungu anatakiwa kuchomwa moto

    ReplyDelete
  6. HAAA KWENI NI HUYO TU MBONA WAKO WENGI NA WALE WALIOKUWA WAKITAPELI NA KINA PAPAA MSOFI NA MZAMIRU TENA MAMILLION YA MAPESA MBONA HASEMI? HUYO MZUNGU NI MSELA HANA SEHEMU YA KULALA NDIO MAANA ANAKWENDA HOVYO KWENYE MABAA KINONDONI AKIKOSA KULIPUA ANALALA KWA MACHANGUDOA, MIMI NAMJUA HANA UHALIFU HUO ANAKUOMBA UKIMPA SAWA UKINYIMA HATUMII NGUVU . MAISHA HAYO!

    ReplyDelete
  7. Ndio mkome maana kuna mijitu ikishamuona hiyo mizungu basi chochote anacho mwambia linakubali pasipo kufikili mijinga sn nyie mnaolizwa.

    ReplyDelete
  8. Hahahahahah!!!

    Mdau wa kwanza mara zote ''Mla kunde huwa rahisi kusahau lakini Mtupa maganda hawezi kusahau''

    Wa-west Afrika na Watanzania wamesha fanya Maafa makubwa sana Ulaya na Marekani.

    Na sasa Wazungu nao wanalipiza Kisasi.

    Tukumbuke ya kuwa Mwosha huoshwa!

    ReplyDelete
  9. Ebwana eee!

    Sisi upigaji wetu ulikuwa ni ule ule wa kuunga unga na labda kwa Msaada wa HIRIZI na TUNGULI kidogo!

    Duuu 'Mibao ya Kupigwa' kwa kulipiziwa Kisasi ya Wazungu mbona tutakoma?

    Sasa Mzungu mwenye kila kitu ktk Sayansi na Tekinolojia HUKU AKIWA ANAAMINIKA KIRAHISI SANA KULIKO SISI si ndio tutafikia Kupigwa na Wazungu hadi kuuzwa kama Ng'ombe na Bata?

    ReplyDelete
  10. Hili ni JEMBE ULAYA Kiboko yao!!!

    Tena Mzungu Nampa Assalam Aleko zake kwa kuianzia Operesheni yake kule kule kulikoungua Mpini na jembe likabaki KINONDONI kwenye Makao Mkuu ya Wasanii wa Mjini.

    Ninyi Kinondoni si ndio mnao jiita na kujifanya Watoto wa Mjini? mie akuu nakaa kwetu Mbagala nimekomboka, vipi tena mnalalamika kugandamizwa nao?

    Jembe Ulaya !

    ReplyDelete
  11. Ohooo !

    Hodi hodi Yanga S.C wana Jangwani, mmeona Shabiki wenu KIVULI, NYATU NYATU huyo anajipanga?.

    Mmeona Flana aliyovaa?, ina Rangi za Yanga na alama ya Afrika ya Yanga!!!

    Baada ya Kinondoni MZUNGU akishawacharaza anakuja Klabuni Yanga!!!


    Akifika atafanya hivi:

    1.Ataghushi Hati za Jengo la Klabu.

    2.Ataghushi Mikataba ya wachezaji wooote na Makocha.

    3.Ataghushi ktk Nyaraka za Vikao na kujiweka kama Raisi wa Klabu.

    BAADA YA HATU HIZO 3 HAPO JUU ATAIUZA KLABU YA YANGA KWA NCHI ZA NJE ATAKOMBA FEDHA KWA KULIPWA KTK AKAUNTI YAKE HUKO KWAO KWA NJIA YA MTANDAO.

    HALAFU ATATOROKA KWENDA NCHI YEYOTE KWA KUWA YEYE HAOMBI VISA KAMA MARAISI WA KLABU ZA YANGA NA SIMBA KAMA AKINA LLOYD NCHUNGA NA ESMAEL ADEN RAGE, MZUNGU HUYOOO ATAHAMIA VISIWANI KULA BATA!

    ReplyDelete
  12. Na huyu jamaa kichwa cha nazi kweli.Hugh mzungu ana ikichwa?wacha kuwa mshamba

    ReplyDelete
  13. huyo jamaa ndio kwaidayake sio mzungu kweli nimzungu warang ,anakaa kinondoni kwamanyanya mtaa furani hunainyeshwa mpira hapo sehemu kumeandikwa chelsea anaitwa john mama yake nimzungu nz babaya mswahili mama yake mwalimu mkuu washule anayomiliki baba yake wakambo na huyo babayake wakamba ni dr mstaafu pia nimteja wa kuvuta unga kama hujui anajifanya kuongea kingereza

    ReplyDelete
  14. Henhe henhe hen!

    Mzungu ametumia akili ameunda hadi Madege, Mitambo na Magari halafu leo anakuja zidiwa akili na Mtanzania na kwa kwa miaka mingi tu amekuwa akitapeliwa na akilizwa?

    Ndio amaana jamaa Mzungu akaona aje Tanzania kuja kujibu mapigo!

    ReplyDelete
  15. Kinondoni mmemuona 'Kinyozi' wenu wa Kizungu huyo?

    Ohhh Mzungu ameona aanzie Kinondoni KUWAPIGA MIKWAJU kwa kuwa ndio kuna idadi kubwa sana ya Wasanii wa Mujini!!!

    ReplyDelete
  16. Kinondoni mwaka huu na Usanii wenu mtakoma!

    Mzungu atawa bonyeza na kuwagandamiza zaidi KIDIJITALI !

    ReplyDelete
  17. Tukumbuke hapo ni Kinondoni 'Shamba la Tanzania' hapo ni Brazil ya Tanzania.

    Mzungu huyo atakuwa TEJA!

    ReplyDelete
  18. Kikubwa kinacho tugharimu Watanzania Wakonongo ni kuwaamini sana na kuwapa nafasi Wageni hasa watu weupe.

    Angalieni leo hii haya yanajiri Tanzania pekee dunia nzima hakuna nchi inayotoa ubwete kwa wageni kama Bongo.

    1.Mabenki yanatoa Fedha kirahisi sana kwa Wageni hasa weupe.

    2.Idara za Mamlaka zipo legevu sana kwa wageni hasa weupe.

    3.Ktk jamii zetu mitaani Wageni hasa weupe wanaaminika sana na kirahisi rahisi.

    Nakwambia kwa Mtaji huo hapo juu (hayo matatu 3) hapa wataliwa wengi sana!

    ReplyDelete
  19. Kutokana na Kinondoni kukomaa kwenu Kiusanii Mzungu ameonelea aje kuwachapa nao awamwage kinyesi na kuzaa na ninyi !

    Jamaa atawa fanyia Usanii hadi mkome.

    Mtazaa na Mzungu !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...