Mhe. Modest J. Mero, Balozi wa kudumu, Ubalozi wa Tanzania, Geneva alipokutana na Bi. Jan Beagle, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na UKIMWI (UNAIDS), katika ofisi ya ubalozi wa Tanzania. Bi. Jan pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Bi. Jan alimtembelea Balozi kwa lengo la kumtaarifu juu ya majukumu ya bodi ya UNAIDS. Hii pia ni muendelezo wa mikutano ambayo Mhe Balozi anafanya na wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye makao makuu hapa Gevena, Uswisi.

Tanzania itakuwa moja wa wajumbe 22 wa bodi ya UNAIDS kwa mwaka huu 2014 kwa kipindi cha miaka mitatu hadi 2016. Katika mazungumzo, umuhimu wa kuendelea kuipa kipaumble mikakati ya kuzuia maambukizo mapya ya UKIMWI yalijadiliwa. 
Msimamo wa Tanzania katika kupambana na janga hili la UKIMWI uliwekwa bayana. Bi Jan alisifu juhudi za Serikali ya Jamuhuri ya Tanzania katika kukabiliana na janga hili, ikiwa ni pamoja na juhudi za serikali inazo fanya kuchangia gharama  kwa kuwa na mpango wa kuanzisha mfuko wa fedha wa kupambana na UKIMWI- AIDS  Trust Fund(ATF).  Mhe Balozi alimhakikishia Bi. Jan kwamba, Tanzania itatoa ushirikiano  wa kutosha katika ushiriki wake kwenye  bodi ya UNAIDS.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...