THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
       P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
                                                                                      
TAARIFA KWA UMMA

Uingereza inajivunia kuwa nchi inayoongoza katika uwekezaji nchini Tanzania na itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kiuchumi na kuleta maendeleo .

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amemuambia Rais Kikwete wakati wa mazungumzo yaliyofanyika 10 Downing Street,  Leo tarehe 31 March, 14, ambapo ndipo yalipo Makao Makuu ya Waziri Mkuu wa Uingereza.

"Tunafurahia sana uhusiano wetu na kujivunia kuwa tunaongoza katika
Uwekezaji nchini Tanzania" Bw. Cameron amesema na kumhakikishia Rais Kikwete kuwa Uingereza iko tayari kutoa misaada zaidi.

Rais Kikwete amewasili nchini Uingereza tarehe 30 Machi, 2014 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku 3 kufuatia mualiko wa Bw. Cameroon ambaye pia amemuomba Rais Kikwete aendelee kutoa mchango wake wa mawazo katika masuala ya kimataifa hasa baada ya mwisho wa muda wa malengo ya millennium ya 2015.

"Tunakaribia mwisho wa muda wa malengo ya millennia Mwaka 2015, tutahitaji kuweka vipaumbele vingine baada ya hivyo kama kuondosha umaskini, Maji safi na salama, masuala ya ufisadi na utawala bora, natumaini utaendelea kutoa mchango wako baada ya malengo hayo kufikia tamati" Waziri Mkuu Cameron amemuambia Rais Kikwete ambapo Rais amekubali ombi hilo na kuahidi ushirikiano wake.

Mapema leo asubuhi Rais amekutana na mtoto wa Mfalme Prince Andrew katika makazi ya Malkia ya Buckingham ambapo wamebadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali ya Kimataifa na Kijamii.

Kabla ya kwenda Buckingham Rais amefungua mkutano kuhusu uwekezaji na kuelezea fursa na nafasi zilizopo za uwekezaji nchini Tanzania na kuelezea kwanini wawekezaji watakuwa wanafanya uamuzi bora kwa kuwekeza Tanzania kuwa ni pamoja na;

"Fursa nyingi, amani, usalama, soko la kutosha na kubwa kwa vile Tanzania iko katika Umoja wa Afrika Mashariki, Ukanda wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika,hivyo kuwa na uhakika wa soko kubwa na pana" amesema.

Katika ziara yake Rais pia amekutana na Mstahiki Meya  wa Jiji la London Mama Alderman Fiona Woolf na kukaribishwa rasmi Jijini London. Mstahiki Meya  anatarajia kutembelea Tanzania, Mwezi Septemba Mwaka huu.

Rais alipowasili London tarehe 30 Machi,2014, alikutana na Watanzania wanaoishi nchini Uingereza na kuwaeleza maendeleo yaliyopo nchini Tanzania.

Rais anaendelea na ziara yake nchini Uingereza

Mwisho.

Imetolewa na;
Premi Kibanga.
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
London Uingereza
31 Machi, 14

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Who is the meya of london jamani?

    ReplyDelete
  2. Not sure, did they get a new one?

    ReplyDelete
  3. Ni Meya of City Of London ni tofauti na Meya wa London ni Boris (Greater London)

    Greater London inajumuisha meya wa borough zote ikiwemo City of London).

    Wakati City of London ni kasehemu kadogo lakini tajiri ndani ya Jiji la London (Mjini kati) ambapo mabeki, taasisi za fedha kubwa duniani zinapatikana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...