Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati) akipokea maandamano ya wadau mbalimbali wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya mazingira jijini Dar es salaam.Kulia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa. 
Baadhi ya wananchi na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakiwa kwenye maandamano huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa kilele cha wiki ya mazingira duiniani leo.

Kikundi cha ngoma za asili kutoka shule ya msingi Umoja kikitoa burudani wakati wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira yaliyofanyika katika uwanja wa Mnazimmoja jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wafanyakazi na wadau wanaojihusisha na shughuli za usafi na usimamizi wa mazingira jijini Dar es salaam wakiwa na zana zao za kazi wakati wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira yaliyofanyika katika uwanja wa Mnazimmoja jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2014

    hivi mimi nauliza kila kukicha huko nyumbani tunasherehekea kwa vishindo siku hiiau ile duniani, lakini huku nje tuliko hakuwi na mapirika hayo, jee hizi kweli ni sherehe za dunia nzima au ni za huko nyumbani tu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2014

    dunia yako si inaanzia nyumbani kwako....kwani kuadhimisha wiki ya mazingira, na hasa kama uko ujumbe muhimu wa kuboresha mazingira kitaifa, ni lazima iwahusu Marekani na Uingereza? Mbona hii iko obvious tu hii inahitaji kufikiri mpaka uelewe.....wewe (mdau hapo juu)uko nje ya dunia gani ambao ustawi wa mazingira kwao siyo priority?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2014

    Westerners hawasherehekei siku hii kwa sababu kwao hakuna uchafu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2014

    Si unajua uchafu siku hizi halimashauri zimeacha shughuli hiyo kwa watu binafsi zamani tulikuwa na magari ya kuzoa taka na hata mapipa ya kuwekea taka tulikuwa tanapata kutoka halimashauri za wilaya na yalikuwa yanapita kwenye eneo lako mara moja kwa wiki, kwa hali hii ya sasa ni lazima wakumbushane vinginevyo hali itakuwa mbaya sana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2014

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...