WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali ina mpango wa kujenga reli mpya ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kupitia mikoa na ya kati na kuelekea Isaka hadi Burundi ambayo ujenzi wake utazinduliwa rasmi Desemba, mwaka huu. 
 Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Julai 10, 2014) wakati akijibu maswali kutoka kwa Watanzania waishio Reading katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Crowne Plaza. Waziri Mkuu ambaye alitumia usafiri wa treni kwenda na kurudi mji wa Reading kutoka London, alisema ni mara yake ya kwanza kufika kwenye mji huo na akaahidi katika siku za usoni kufanya mikutano ya aina hiyo kwa Watanzania waishio kwenye miji mingine ya Uingereza kulingana na ratiba ambayo watu wa ubalozini watakuwa wameipanga. 
 “Kuna mtu ameulizia kuhusu tatizo la usafiri nchini Tanzania, napenda kuwahakikishia kwamba Serikali imeamua kuwekeza kwenye mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kati. Reli hii itaanzia Dar es Salaam hadi Isaka, Isaka hadi Burundi; itatokea Tabora hadi Kigoma na Tabora hadi Mwanza pamoja na kipande cha Kaliua hadi Mpanda,” alisema. 
 “Mradi huu ni mkubwa ambao ujenzi wake utagharimu dola za marekani bilioni saba, na utatuchukua karibu miaka minne. Kwa hiyo ikiifika Desemba, mwaka huu utafanyika uzinduzi rasmi kwa njia zote hizi za reli,” alisisitiza Waziri Mkuu. 
 Alisema ili kufanikisha ujenzi Serikali imeamua kujenga upya reli ya kati kwa standard gauge hali ambayo haitaathiri usafiri wa treni kwa kutumia njia ya zamani. “Safari hii tumeamua kujenga upya, na siyo kubanduabandua ili wakati reli mpya ikiendelea kujengwa na ile ya zamani inaendelea kutoa huduma kama kawaida,” alisema huku akishangiliwa. 
 Maswali mengine aliyoulizwa Waziri Mkuu yalihusu ujenzi wa barabara ya Lindi-Mtwara, ujenzi wa hospitali ya Kagwa, ujenzi wa uwanja wa ndege wa Musoma, utaratibu wa utoaji wa mizigo bandarini na usumbufu wanaoupata, uraia wa nchi mbili, tatizo la walimu na hali ya elimu nchini ambayo yote aliyajibu na kuahidi kufuatilia masuala mengine akifika nyumbani.
 Kwa ujumal, Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waishio nchi za nje (wana Diaspora) kufuatilia kwa makini mikutano ya uwekezaji (Investors’ Forums) ambayo hufanyika kwa kanda au kwa mikoa ili iwasadie kubaini fursa za uwekezaji zilizoko kwenye mikoa wanayotoka.
 “Tumieni fursa hizi, zitawasaidieni kubaini kwa haraka ni maeneo gani mnaweza kuwekeza kwa haraka. Kama Diaspora mnaweza pia kutumia kipengele cha utalii wa Tanzania kutusaidia kuitangaza nchi yetu,” alisema Waziri Mkuu. 
 Waziri Mkuu jioni hii (Jumamosi, Julai 12, 2014) amekutana na Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano uliofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania, jijini London.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akipanda treni kutoka Reading kwenda London Uingereza baada ya kuzungumza na watanzania waishio Reading Julai 10, 2014. 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu  (kulia) wakiongozana na Madona Pemba (kushoto) , mtanzania aishie Uingereza kuelekea kwenye ukmbi wa mikutano  ili kuzungumza na watanzania waishio Reading Julai 10, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu  (kulia) wakisalimiana na baadhi ya watoto na wazazi  waliohudhuria mkutano kati yake na watanzania waishio Reading Uingereza Julai 10, 2014   
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi ya mipira  kutoka kwa watanzania waishio Reading nchini Uingereza  kabla ya kuzungumza nao Julai  10, 2014. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania waishio Reading, Hussein Chang'a.  
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2014

    Siamini. Huko UK hakuna magari ya vimulimuli kama hapa?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2014

    Kupanda treni ni kawaida. Ni bongo tu ndiyo utaona kila kiongozi anapewa gari na dereva.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2014

    Wenzenu wabunge wanaenda ofisini na bike

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2014

    Na kumbuka kwamba train za huku si kama za bongo!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 12, 2014

    IGENI MFANO YA HUKO MLETE TZ, KWANI TUNACHANGA MOTO KUBWA YA FOLENI, NA HATUJAONA VIONGOZI WETU WAMEFANYA NINI MPAKA SASA HIVI KUTATUA TATIZO HILI KUBWA MNO KWA WAKAZI WA DAR. VIONGOZI WETU MUWAPO ZIARANI HUKO MSIHISHIE KULA BATA!! KWA KWELI WATANZANIA TUNAISHI ZAMA ZA MAWE, HATA HUU MWENDO KASI NAONA KAMA NDOTO BILA FLYOVERS ITAKUWAJE, NA MWENDO KAZI WENYEWE UTAPITA WAPI KAMA HATA TRAMS HAKUNA, TRENI KAMA HUKO HAKUNA, MABASI NDIO USISEME.

    SI SHANGAI WAZIRI WETU KUPANDA TRAIN KWA NDIO USAFIRI MKUU NA WAHARAKA KWA NCHI ZA WENZETU,LAKINI NYIE WABONGO MLIOKO HUKO WASAIDIENI VIONGOZI WETU KULETA MABADILIKO, MSIFURAHIE KUISHI HUKO NA KUONA HAYO NDIO MAISHA, WAZUNGU WAMEJENGA NCHI ZAO NA NYIE MTATUSAIDIA LINI TUIJENGA TZ?!!!!TUNAZIDIWA NA KENYA LOLOO.... AIBU TU, BARABARA ZOTE ZEROOOOOOOOOOO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...