Mratibu wa Wiki ya Ujasiriamali Tanzania, Lilian Secelela Madeje (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maandalizi ya wiki hiyo inayotarajiwa kuanza Novemba 17 mwaka huu jijini humo. Kutoka kushoto ni mmoja wa wajasiriamali, Mboni Masimba wa kipindi cha Mboni Show na Meneja Miradi na Biashara wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Magabe Kibiti Maasa.
Meneja Miradi na Biashara wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Magabe Kibiti Maasa (kushoto) akizungumza kuhusu kushiriki kwa DSE katika maadhimisho ya Wiki ya Ujasiriamali Tanzania yanayotarajiwa kuanza Jumatatu ijayo jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto kwake, ni Mratibu wa Wiki ya Ujasiriamali Tanzania, Lilian Secelela Madeje ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Professional Approach Development na Meneja Mradi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Rukia Lukanza.
Mmoja wa waanzilishi wa asasi ya KINU, Emanuel Feruzi (kulia) akizungumza kuhusu ushiriki wao katika maadhimisho ya Wiki ya Ujasiriamali Tanzania. Kulia kwake ni Rukia Lukanza wa ILO na mratibu wa wiki hiyo, Lilian Secelela Madeje.
Mmoja wa wajasiriamali, Mboni Masimba (kushoto), wa kipindi cha Mboni Show anayetarajiwa kuwa mmoja wa watoa mada katika semina na mikutano wakati wa Wiki ya Ujasiriamali Tanzania akizumguza katika hafla hiyo. Kushoto kwake ni Meneja Miradi na Biashara wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Magabe Kibiti Maasa na mratibu wa wiki hiyo, Lilian Secelela Madeje.
Baadhi ya waratibu, wadhamini na waandishi wa habari wakiwa katika hafla ya utambulisho wa maadhimisho ya tatu ya Wiki ya Ujasiriamali Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...