Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi na wanachama wa chama hicho,waliofika kwa wingi katika mkutano wa hadhara,wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika jimbo la Mpendae,wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi.Ndugu Kinana kabla ya kuhitimisha ziara hiyo alishiriki kazi za kijamii na kukagua miradi mbalimbali ya chama.
Sehemu ya umati wa Wakazi wa wilaya ya Mpendae na wanachama wa CCM wa jimbo la Mpendae,wilaya ya Amani,Mkoa wa Mjini Magharibi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Binti Amran Mpendae,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika Wilaya ya Amani,mkoa wa Mjini Magharibi. 

 katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwalisha kiapo baadhi ya wanachama wapya walijiunga na chama hicho sambamba na kukabidhiwa kadi za uanachama.
 Sehemu ya viongozi mbalimbali wa chama cha CCM wakishangilia jambo katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa Binti Amrani Mpendae,wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Vuai Ali Vuai akisoma baadhi ya vifungu vilivyomo kwenye katika inayopendekezwa mbele ya wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara,uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Binti Amrani Mpendae,Wilaya ya Amani,mkoa wa Mjini Magharibi. 
katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi na wanachama wa chama hicho,waliofika kwa wingi katika mkutano wa hadhara,wakati Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika jimbo la Mpendae,wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi.Nape pia aliipongeza kazi nzuri inayofanywa na Dkt shein ya kuimarisha chama,amewataka viongozi mbalimbali wa chama hicho kuiga mfano wake,pia amewataka viongozi wa chama hicho kuacha kuwa na majivuno badala yake watoke na kukutana na wananchi kuwasikiliza na kuwatatulia matatizo yao kwa namna moja ama nyingine.
 Mkutano ukiendelea katika uwanja wa Binti Amrani Mpendae,Wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi jioni ya leo.
 Sehemu ya umati wa Wakazi wa wilaya ya Mpendae katika jimbo la Mpendae,wilaya ya Amani,Mkoa wa Mjini Magharibi wakifautilia yaliyokuwa yakijiri katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Binti Amran Mpendae,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake katika Wilaya ya Amani,Jimbo la Mpendae mkoa wa Mjini Magharibi.
PICHA NA MICHUZI JR-ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...