Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
JAMII imeaswa kuunga mkono juhudi mbalimbali dhidi
ya mapambano ya ukosefu lishe bora kutokana na kudumaza watoto na kushindwa taifa
kupata nguvu kazi katika jitihada za kusukuma uchumi.
Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa
Masuala ya Lishe pamoja na Haki za Watoto,Lediana Mng’ong’o wakati akizindua
ripoti lishe Duniani iliyokutanisha nchi mbalimbali kwa ajili ya kuweza kupata
nguvu katika kupambana na lishe, iliyofanyika leo katika Hoteli ya Protea, Jijini Dar
es Salaam.
Lediana amesema kuwa katika mapambano ya lishe inahitajika
kuwa na sauti moja katika kuzungumzia suala hilo ikiwa
ni pamoja na kushirikisha viongozi wa vyama pamoja wabunge.
Amesema suala hili likipewa utashi wa kisiasa kama
yeye alivyojitoa katika mapambano na jitihada za watu wengine kuna uwezekano wa
kupunguza tatizo la lishe lililopo sasa.
Aidha amesema hali ya lishe kwa mwaka 2010 watato
waliodumaa kwa lishe ilikuwa asilimia 42 lakini kutokana na jitihada za
mapambano hayo imefikia asilimia 35.
Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Lishe Tanzania(PANITA),Tumaini
Mikindo amesema kuwa sasa ni wakati wa kuweka mkazo wa kuwepo bajeti za masuala
ya lishe kuanzia katika ngazi ya kata katika kupunguza utapiamlo.
Amesema
kutokana na ripoti hiyo na wadau walioshiriki wakiwemo viongozi wa vyama vya
siasa ni hatua nyingine katika kuongeza kasi dhidi ya mapambano ya lishe
nchini.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Masuala ya Lishe pamoja na Haki za Watoto,Lediana Mng’ong’o akizungumza na wadau wa masuala ya lishe kwa watoto wakati wa kuzindua ripoti ya masuala ya lishe Duniani katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa ushirikiano wa lishe Tanzania (PANITA), Tumaini Mikindo akifafanua jambo katika uzindua wa Ripoti ya masuala ya lishe Duniani leo katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa ushirikiano wa lishe Tanzania (PANITA), Tumaini Mikindo akifafanua jambo katika uzindua wa Ripoti ya masuala ya lishe Duniani leo katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa masuala ya lishe nchini Burundi, Jean Nkurunziza akitoa mchango wake kuhusiana na masuala ya lishe nchini Burundi katika mkutano wa kuzindua ripoti ya masuala ya lishe Duniani iliyofanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za watoto Tanzania(TAJOC),Chalila Kibuda akiweka saini juu ya mapambano ya lishe katika uzinduzi wa ripoti ya Lishe Duniani iliyofanyika leo katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
Wadau wa lishe wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wameshika Ripoti ya Lishe Duniani mara baada ya kutoka katika mkutano wa uzinduzi wa Ripoti hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Kampeni za chakula bora, chanjo, elimu ya watu wazima, na uchimbaji vyoo au mtu ni afya zilikuwepo toka miaka ya sabini zianzishwe upya na taasisi husika katika kila wilaya.
ReplyDelete