Mkuu wa Biashara za Kibenki, Rahim Kanjii
akipeana mkono na Mwalimu
Mkuu wa Shule ya msingi Chamanzi, Ancent Shayo mara baada ya kutoa msaada wa meza 25 na viti 25.
Na Chalila
Kibuda,Globu ya Jamii
BENKI ya NIC imetoa msaada wa madawati 25
katika shule ya msingi Chamanzi yenye thamani ya Sh.Milioni tatu kutokana na
shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya madawati.
Akizungumza
baada ya kukabidhi madawati hayo, Mkuu wa Biashara za Kibenki,Rahim Kanjii
amesema kuwa shule hiyo waliona ina umhimu wa kusaidiwa sehemu ya madawati
katika kupunguza idadi ya wanafunzi wanaokaa chini ardhi wakiwa darasani.
Amesema
shule hiyo inatakiwa kusaidiwa kwa kila hali kwani watoto wanaoandaliwa kuwa
taifa la kesho hivyo wanatakiwa kuandaliwa mazingira bora ya kupata elimu.
Kanji
amesema kuwa ameguswa sana na benki itaendelea kadri ya uwezo wake kusaidia
shule katika kuweza kuondokana na chagamoto ya madawati katika kujenga mazingira bora ya kusomea
watoto kwani wanaandaliwa kuja kuwa wanataaluma mbalimbali.
Naye Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo, Ancent Shayo amesema kuwa shule ina wanafunzi 3200 lakini
vyumba vya madarasa 11 na kufanya kila darasa kukaa wanafunzi 150.
Amesema
madawati hayo ni kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne kutokana na kupungukiwa madwati 175 ambapo NIC imepunguza imetoa madawati 25 hivyo kwa darasa hilo
linahitaji madawati 150 ili waweze kukaa katika siku ya mtihani wa taifa.
Shayo
amesesema hitaji katika shule licha ya madawati wanaupungufu wa vyumba vya
madarasa kutokana na idadi ya wanafunzi
hao.
Wanafunzai wa shule ya msingi Chamanzi wakiwa darasani wakiwa wamekaa chini kwa kutokuwa na madawati ya kutosha katika chumba cha darasa la tatu walipotembelewa na wafanyakazi wa Benki ya NIC leo jijini.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya msingi Chamanzi, Ancent Shayo akizwa na wafanyakazi wa Benki ya NIC walipowatembelea wanafunzi wa Shule ya Msingi Chamanzi jijini Dar es Salaam walipotembelea chumba cha darasa la kwanza katika shule hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...