Studio party ulikuwa mjumuiko ulioleta furaha kwa wengi kama inavyoonekana katika kiwanja cha Maisha Club
 Baadhi ya mayanki waliohudhuria Coke Studio party wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye ukumbi wa Maisha Club jijini Dar es Salaam.
Ilikuwa ni burudani kubwa vijana wakicheza muziki kwa furaha ndani ya Maisha Club 
Vijana wakishiriki kuimba Coke Studio Party mkoani Mwanza 
 Zawadi mbalimbali zilitolewa katika party ya Mwanza kama anavyoonekana Masai akijichukulia zawadi katika party ya Mwanza.
DJ akinogesha mambo ya Coke Studio mjini Mwanza




Ma Dj walikuwa wakifanya mambo kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri 
Watu wa rika mbalimbali walifika CokeStudio party kupata burudani kama wanavyoonekana baadhi yao pichani mjini mwanza.

 Mamia waburudika na Coke-party ya kukata na shoka
Onyesho la muziki la Coke Studio ambalo linajumuisha Kolabo ya wanamuziki wa kitanzania kwa kushirikiana na wanamuziki wa Nje ya nchi limeanza kurushwa nchini kila  Jumamosi kupitia Luninga ya Clouds ikiwajumuisha wanamuziki mahiri Ally Kiba,Vanessa Mdee,Ben Pol na Fid Q ambao wanashirikiana na wanamuziki Wangechi,Maurice Kirya,Victoria Kimani na 2Face.

Baada ya uzinduzi huo zilifanyika party za kufa mtu katika viwanja vya maraha katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Arusha zilizowajumuisha vijana kucheza muziki,kuimba na kujishindia zawadi mbalimbali za Coca Cola

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...