Na RAMADHANI ALI, MAELEZO ZANZIBAR                                    
 Chama cha Wanasheria Mawakili Zanzibar kimepata heshma ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa siku mbili wa mwaka wa Wanasheria Mawakili wa Nchi za Afrika Mashariki utakaoanza  tarehe 27 Mwezi huu katika Hoteli ya Sea Cliff Resort.
Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Bwawani, Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria Mawakili Zanzibar Omar Said Shaaban amesema mkutano huo utawashirikisha zaidi ya Wanasheria 400 kutoaka Nchi zote wananchama wa Afrika Mashariki na Mataifa mengine Duniani.
Amesema kwa kawaida Jumuiya ya Wanasheria Mawakili wa Nchi za Afrika Mashariki inawachama wa aina mbili ambao ni wanasheria wenyewe binafsi na Jumuiya za kila Nchi nazo huwa ni mwanachama wa pili.
Katibu Mkuu wa Wanasheria Mawakili Zanzibar amesema Mkutano huo utakuwa na malengo ya kubainisha kuwa Taaluma ya sheria kama kichocheo cha Biashara na Uwekezaji ambapo mada mbali mbali zitawasilishwa.
Amezitaja baadhi ya mada zitakazowakilishwa katika mkutano huo ni pamoja na Kada ya Sheria kama biashara, muundo mzima wa Biashara na uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na mada nyengine ni masuala ya rushwa na vipato visivyohalali.
Ametoa wito kwa wananchi wa Zanzibar kuupokea ugeni huo mkubwa wa wanasheria na kuonyesha ukarimu uliozoeleka kwa wageni na kutumia fursa ambazo zitapatikana kutokana na kuwepo kwao hapa nchini.
Amesema chama kwa upande wake tayari kimeliarifu Jeshi la Polisi kuhusu ugeni huo kwa lengo la kuimarisha hali ya usalama wakati wote wa mkutano.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria Zanzibar amesema Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (pichani) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...