Muogeleaji bora wa dunia wa zamani na bingwa wa kuogelea wa Olimpiki, Penelope “Penny” Heyns amevutiwa na waogeleaji vijana na kusema wakiendeleza kwa kupata mafunzo ya kisasa, Tanzania itatwaa medali nyingi katika mashindano ya kimataifa. 
Penny alisema hayo katika semina ya siku tatu iliyaondaliwa na klabu maarufu ya Dar Swim Club yaliyoafanyika katika hoteli ya Coral Beach, Masaki jijini Dar es salaam.
Alisema kuwa amefarijika kuona waogeleaji wengi chipukizi aliofanya nao semina kama hiyo mwaka jana kuwa na viwango vya juu na kumpa faraja kubwa kuwa siku moja watakuwa waogeleaji bora Afrika na dunia kwa ujumla. 
“Hii ni mara yangu ya pili kufanya semina na Dar Swim Club, nilifanya nao mwaka jana na waogeaji wamepata maendeleo makubwa, ni muhimu kuwaendeleza kwa kupata mafunzo kama haya,” “Nimeambiwa kuwa klabu imepata mafanikio makubwa hapa nchini kwa kushinda medali na kuwa wa kwanza katika mashindano ya Taliss, haya ni matunda ya mafunzo bora,” alisema Penny. 
Penny pia aliipongeza Dar Swim Club kwa kuwa na utaratibu mzuri wa mazoezi na mafunzo na anaamini wataendelea kufanya vyema katika mashindano mbalimbali ya ndani na kimataifa. Mmoja wa waogeaji chipukizi wa klabu hiyo, 
Reuben Monyo alisema kuwa wamepata mwanga mkubwa katika mafunzo hayo na anaona mwanga wa mafanikio katika fani hiyo. Monyo (10) alisema kuwa lengo lake ni kuona Tanzania inafanya vyema na yeye kuwa muogeaji nyota katika hapa nchini na mashindano makubwa kama Jumuiya ya Madola na Olimpiki. Kocha mkongwe wa mchezo huo hapa nchini, 
Ferick Kalengela alisema kuwa mafunzo ya Penny yamewapa mbinu mpya katika mchezo huo na wana uhakika wa kufanya vyema hapa nchini na katika mashindano ya kimataifa. “Tumepata mafunzo mazuri tena ya kisasa, lengo letu ni kuona tunafika mbali katika mchezo na hasa kupitia msemo wetu, 
“Tunataka kila Mtanzania ajue kuogelea”,alisema Kalengela. Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro alisema kuwa Wameandaa mafunzo hayo kwa lengo la kuendeleza mchezo huo hapa nchini mbali na klabu yao. 
Inviolata alisema kuwa wanajua umuhimu wa mafunzo kama hayo na kusaka wadau kusaidia ili kufanikisha pamoja na changamoto mbalimbali walizokutana nazo. “Maendeleo ya Dar Swim Club ni maendeleo ya mchezo huo hapa nchini, tunaamini kuwa tukifanya vizuri sisi, sifa itakuwa kwa nchi nzima,” alisema.
 Wachezaji wa klabu ya Dar Swim Club wakijiandaa kuanza kuogelea kwa kufuata malekezo ya bingwa wa zamani wa Olimpiki na Muogeleaji bora wa kike, Penny Heyns (hayupo pichani) katika  mafunzo yaliyofanyika Masaki jijini.
 Bingwa wa zamani wa Olimpiki na Muogeleaji bora wa kike, Penny Heyns (watatu kutoka kulia) akitoa somo la jinsi ya kuogelea kwa spidi kwa makocha na waogeleaji wa Dar Swim Club katika mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika Masaki.
 Makocha wa mchezo wa kuogelea wa klabu ya Dar Swim Club  wakiwa darasani kumsikiliza bingwa wa zamani wa Olimpiki na muogeleaji bora wa kike duniani, Penny Heyns  katika semina iliyofanyika kwenye hotel ya Coral Beach jijini.
 Bingwa wa zamani wa Olimpiki na Muogeleaji bora wa kike, Penny Heyns (kulia) akielekeza jambo kwa mmoja wa makocha wa klabu ya Dar Swim Club, Radhia Gereza katika mafunzo yaliyofanyika Masaki jijini.
Bingwa wa zamani wa Olimpiki na Muogeleaji bora wa kike, Penny Heyns (wa pili kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na makocha wa klabu ya Dar Swim Club mara baada ya mafunzo yaliyofanyika Masaki jijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...