Mkutano ulifanyika katika ofisi ya TIRDO ambayo ni Taasisi tanzu ya Wizara ya Viwanda na biashara, ambapo kulishuhudiwa utiwaji saini wa makubaliano kati ya GS1 Tanzania na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika kushirikiana kufanya kazi pamoja na kujenga mahusiano ambayo ni muhimu haswa kwa wazalishaji wa Tanzania kwani alama ya utambuzi wa bidhaa kwa sasa zinahitajika katika masoko yote ya ndani na nje ya nchi.
TBS imekua ikishirikiana na GS1 Tanzania katika uelimishaji wajasiliamali ambayo mafunzo kadhaa kati ya Taasisi hizi mbili yameshafanyika huko mkoani.
Wazalishaji wa Tanzania wanaotumia Barcode za nje ya nchi wanaaswa kubadilisha na kutumia Barcode(alama za uzalishaji) za hapa nchini kwani itasaidia::
  • Kupunguza matumizi ya fedha za kigeni ambazo zingetumika kulipia huduma hiyo.
  • Kutupa takwimu rasmi za wazalishaji kwani kutumia barcode za nje ya nchi bidhaa inaonekana imetoka kwenye nchi nyingine na sio Tanzania.
  • Kuwepo kwa utambulisho kwa bidhaa za Tanzania kwani nambari tatu za mwanzo za Barcode zinaonyesha bidhaa zinatoka nchi gani, ambapo kwa bidhaa za Tanzania utambulisho wetu ni 620.
  • Mwisho ni suala zima la uzalendo, tujivunie cha kwetu.
Kuna wazalishaji wa Tanzania 13 tu ambao wamechukua alama za uzalishaji (barcode), sio tu wameonesha uzalendo bali wameendana na matakwa ya masoko yaliyo rasmi ya ndani na nje ya nchi. Huduma hii kama umekamilisha matakwa yote unaipata ndani ya siku moja tu.
GS1 Tanzania inahudumia nchi zaidi ya tano ambazo hazina huduma hii nazo ni Rwanda, Burundi, Uganda, Zambia, Malawi na Mozambique.
GSM 1 Tz-30
Mwenyekiti wa bodi GS1 Tanzania Dr. Gedion Mazara alifungua kikao kwa kuelezea kuhusu alama za utambulisho (barcode) na umuhimu wake.
GSM 1 Tz-38
Mkurugenzi mkuu wa GS1 Tanzania pia aliongelea ni jinsi gani wazalishaji wakipata na kutumia barcode/alama za uzalishaji itasaidia sana nchi
GSM 1 Tz-47
Mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Uhamishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. The mdudu, yaani mpaka Leo hii bado watu wanatumia BARCODE za nchi za nnje? amakweli Tanzania bado tuko nyuma sana watu 13 tu Tanzania nzima ndio wanao tumia Barcode za Tanzania ndio maana hapa nilipo England Kwa mama nishida kuona vitu vyangu vya kitanzania yaani hata nembo ya TBS ni shida loh poleni sana viongozi wa mashilika ya umma ndio maana muheshimiwa JPM ana watumbua bila ganzi hiyo MIJIPU sawa sawa kabisa tumbua muheshimiwa rais John Pombe Magufuli watanzania wote hapa uingereza tunakuunga mkono hata mambo ya uchadema na Ukawa tumevizika kabisa havipo tena

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...