Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU ya netiboli ya Uchukuzi SC jana ilianza vyema mchezo wake wa kwanza kwa kuwaicharaza CDA ya
Dodoma katika mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea mkoani Dodoma.
Uchukuzi SC inayoundwa na wachezaji wakongwe, akiwemo mfungaji mahiri wa timu ya Bandari na
Taifa, Matalena Mhagama waliwapeleka puta wapinzani wao ambapo hadi mapumziko walikuwa mbele
kwa magoli 11-6.
Katika mchezo huo uliokuwa umetawaliwa na rafu za hapa na pale na kulalamikiwa mara kwa mara na
wachezaji wa Uchukuzi SC, ulimalizika kwa mfungaji Matalena kufunga magoli 16 na Tatu Kitula akifunga
saba, wakati wapinzani wao Tatu Fungo nma Margeth Nicholaus kila mmoja akifunga magoli nane.
Kocha Mkuu wa Uchukuzi SC, Judith Ilunda alisema wamepata ushindi huo wa kwanza kutokana na
kufanya mazoezi ya pamoja ya muda mrefu, pamoja na kwamba wapinzani wao walikuwa ni wazuri na
wenye uzoefu mkubwa.
“Wengi waliocheza na kikosi change ni wakongwe wapo niliocheza nao mimi kwenye mashindano
mbalimbali, hivyo wameweza kutumia ukongwe wao lakini tuliwazidi mbinu kutokana na timu yetu
kuundwa na chipukizi wengi,” alisema Ilunda.
Lakini, alilalamikia maamuzi ya waamuzi waliocheza mchezo huo kuwa mengi yamepitwa na wakati
kutokana na sheria kubadilika mara kwa mara.
“Hawa waamuzi wamekuwa wakichezeshakwa sheria nyingi za zamani na kusababisha mvutano, hivyo
wanatakiwa wabadilike kwa kujisomea mara kwa mara ili kuondoa mkanganyiko kwa timu zinazocheza,”
alisema Ilunda.
Hatahivyo, waamuzi Mariam Makisi na Caroline Paulo wote wa Dodoma, kwa nyakati tofauti walisema
wamechezesha mchezo huo kwa kanuni na sheria za mchezo huo, lakini wameshangazwa na malalamiko
ya kuwa wamechezesha kwa sheria za zamani.
“Unajua timu za Dar es Salaam siku zote zinajifanya kujua sheria zaidi, na wangeweka wazi ni wapi
waamuzi tulipopindisha sheria,” alisema Makisi.
Wakatihuohuo, timu ya Tamisemi iliwafunga TPDC kwa magoli 6-1 katika mchezo wa soka uliofanyika
kwenye uwanja wa Jamhuri.
Wafungaji wa Tamisemi ni Mwigane Yeya kafunga magoli mawili, wakati waliofunga moja-moja ni Hamis
Shedafa, Hamad Majura, Nelson Richard na Phillipo Oden; wakati bao la kufutia machozi la TPDC
lilifungwa na Shija Dalushi.
Katika mchezo mwingine wa soka, timu ya Tanesco ilipata ushindi wa chee baada ya wapinzani wa CWT
ya Dodoma kushindw kutokea uwanjani.
Mfungaji wa CDA Dodoma, Tatu Fungo akiuwahi mpira katika mchezo wao wa
netiboli wa Kombe la Mei dhidi ya Uchukuzi SC. Uchukuzi walishinda kwa magoli 23-16.
Mchezaji Mwadawa Hamisi wa Uchukuzi SC (GK) akiangalia mwenzake wa
kumrushia baada ya Tatu Fungo wa CDA kufunga bao katika michuano ya Mei Mosi. Uchukuzi
walishinda magoli 23-16.
Mchezaji Matalena Mhagama wa Uchukuzi SC (GS) akijiandaa kupokea mpira kutoka kwa Tatu
Kitula aliyezuiwa na Catherine Ukunguala, katika mchezo wa netiboli wa mashindano ya Mei
Mosi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...