Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa Yanga umelaani vikali vitendo vya uvunjivu wa amani vilivyotokea katika mchezo wao dhidi ya GD Sagrada Esperanca vilivyofanywa na mwamuzi wa mechi hiyo na vyombo vya usalama.

Katika mchezo huo Yanga wamefanyiwa vurugu ikiwemo na golikipa wa timu hiyo Deogratius Munish 'dida' kupigwa na mawe na Polisi kuingia uwanjani mara kwa mara.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema kuwa Mwamuzi wa mchezo amefanya vitendo vingi ambavyo havipo katika sheria 17 za soka.

"Mwamuzi amefanya vitendo vingi vya uvunjivu wa sheria za mpira wa miguu ikiwemo kuwatoa wachezaji mchezoni kwa kuwapatia kadi huku upande mwingine wakiwa wanafanya makosa pasi kupatiwa onyo lolote,"amesema Muro. Kwa sasa uongozi umeamua kuandika barua kwa shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) kuomba kuondolewa kwa mwamuzi huyo ikiwemo kufungiwa au kutokuchezesha  mechi zao.

Muro amesema kikosi kipo nchini Afrika kusini kikisubiri ndege ya kesho saa 4asubuhi na kuingia mchana ambapo wataingia kambini moja kwa moja kwa ajili ya safari kuelekea Songea kumalizia mchezo wao dhidi ya Majimaji utakaopigwa Jumapili.

Wakati huohuo.
TFF TUNAOMBA FAINALI FA  ISOGEZWE MBELE - YANGA.
KLABU ya Yanga imeliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kusogeza mbele fainali ya kombe la Shirikisho FA, kwakuwa ratiba ya ligi kuu kuoneana kuwabana.

Awali fainali hiyo ilipangwa kufanyika Juni 11 lakini jana TFF ilibadilisha tarehe hiyo na kusema àassaaaqàa 25 ndiyo itapigwa faainali.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano amesema  wanawaomba TFF kusogeza mbele ratiba hiyo kwani ratiba imewabana hasa ukilinganisha kuwa kikosi chao bado hakijarea na kitakaporejea kitapumzika masaa machache kisha kitaanza safari ya kuelekea Songea kwa usafiri wa gari ambapo masaa zaidi ya 14 watakuwa njiani na watashuka dimbani Jumapili na Jumatatu wataanza safari ya kurudi Dar es salaam.

"Ukiangalia ratiba inabana huwezi kurudi Jumatatu usiku halafu Jumatano tuingie uwanjani kwa ajili ya kombe la FA ambao ni moja ya mchezo muhimu kwetu," amesema. Kwahiyo kwa heshima wanaomba wafikiriwe katika hilo kwani kwakuwa wachezaji watajumuika na timu zao za Taifa basi fainali hiyo inaweza kusogezwa ikasubiri mechi za kitaifa kumalizika.

Kutokana na hilo Yanga wametaka waweze kufikiriwa kulingana na ratiba ilivyo pamoja na hilo serikali inatakiwa kushirikiana na TFF kuweza kuzisaidia klabu pale zinapoenda nje ya nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2016

    Matendo hayo hayo ndio yanafanywa na waamuzi wa ligi ya TZ kwa timu nyingine zikicheza na yanga. Hata hivyo hongereni.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2016


    Yaani wabongo kwa kujilalamisha ndio zao.wao ndio wanaoonewa kila wakienda kucheza nje. kila mara wakienda nje hawakosi lawama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...