KIKOSI cha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17‘Serengeti Boys’

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KIKOSI cha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17‘Serengeti Boys’ kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa goli 6-0 dhidi ya timu ya Shelisheli  na  Ushindi huo unaifanya Serengeti kuwa na jumla ya goli 9-0 baada ya kushinda mchezo wa awali uliopigwa katika uwanja wa Taifa na baada ya kushinda mchezo huo wa kuwania kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika sasa Serengeti itavaana na timu ya Taifa ya Afrika Kusini mwezi ujao.

Mchezo ulianza kwa timu zote kushambuliana lakini Serengeti ilionekana kuutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa huku Timu hiyo ambayo ni wawakilishi pekee wa nchi kwenye mashindano ya kimataifa ilipata goli lake la kwanza dakika ya tisa kupitia kwa Ibrahim Abdallah baada ya golikipa kutema shuti lililopigwa na Asadi Ally.

Serengeti inapata goli la pili lililofungwa na Mohemmed Abdallah dakika ya 43 pale alipoachia shuti kali lililomshinda kipa wa wapinzani wao na kuzama wavuni. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika serengeti walikuwa kifua mbele kwa goli 2 huku wakionekana kuutawala vilivyo mchezo huo wa ugenini.

Kipindi cha pili kinaanza kwa Serengeti kuingia kwa kasi ambayo inazaa matunda dakika ya 50 pale Asad Juma anapoandika goli la 3 baada ya kupiga faulo inayotumbukia moja kwa moja wavuni.Wageni hao katika uwanja wa Stade Linite  wanapata goli la 4 kwa penati dakika ya 61 inayopigwa na Issa Makamba na Asad Juma anaandika bao la tano dakika ya 70 huku Yohana Mkomola akiandika goli la sita dakika ya 90

Kikosi cha Serengeti Boys
Ramadhani Kambwili
Israel Mwenda
Nickson Kibabage
Enrick Nkosi
Ally Msengi
Ally Ng'anzi
Mohameed Abdallah
Shaban Ada
Ibrahim Ally
Rashid Chambo
Asad Juma

Kikosi cha Shelisheli.
Gino Pusureuse
Juninno Mathiot
Stan Estner
Brandon Molle
Mathew Basset
Churtill Rose
Emmanuel Lesperance
Julius Joseph
Ryan Henriette
Aaron Havolock
Brandon Fanchette

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...