Taarifa iliyotufikia inaeleza kuwa, Mwandishi Mkongwe nchini na Mwenyekiti wa Bodi ya Gazeti la Raia Mwema, Jenerali Ulimwengu amepata ajali mapema asubuhi ya leo, na kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa Moi kwa matibabu.
Ajali hiyo imehusisha gari alilokuwa akiendesha yeye aina ya Benz na gari nyingine iliyoigonga gari hiyo upande wa Ubavuni.
Ajali hiyo imehusisha gari alilokuwa akiendesha yeye aina ya Benz na gari nyingine iliyoigonga gari hiyo upande wa Ubavuni.
Mwandishi mkongwe Jenerali Ulimwengu akijuliwa hali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dar es Salaam ambako amelazwa kwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika ajili iliyotokea Mikocheni, Dar es Salaam.
Nakutakia speed recovery mwanamapinduzi Taifa zima bado linahitaji mchango wango muhimu. Pole sana!
ReplyDelete