Moja ya eneo lenye makazi holela katika Jiji la Dar es salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji makazi holela toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Betha Mlonda akifafanua kwa waandishi wa Habari kuhusu mpango wa urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholea katika Jiji la Dar es saaam ambao umeanza kutekelzwa katika eneo la Kimara Jijini humo .kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari- Maelezo Bi Fatma Salum na kushoto ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bw. Hassan Mabuye.
Mmoja wa Wataalamu wa  upimaji Ardhi akiweka alama katika eneo lililorasimishwa.

Fatma Salum-Maelezo.
SERIKALI imeanza kutekeleza mpango wa kutambua, kupanga na kupima vipande vya ardhi na kuweka huduma za jamii kama miundombinu ya barabara na mitaro ya maji ya mvua ili kuboresha mazingira ya makazi na kuongeza usalama wa miliki kwa kutoa hatimiliki. 

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Makazi Holela kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi. Bertha Mlonda wakati wa mkutano na vyombo vya habari.

Akifafanua Mlonda alisema kuwa mpango huo unatekezwa kwa kushirikiana na Halmashuri zote za Jiji la Dar es salaam na tayari zoezi limeanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambapo wananchi wameonyesha mwitikio mkubwa kwa kuunga mkono juhudi hizo za Serikali.

Akizungumzia vigezo vinavyofuatwa katika urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela, Mlonda alibainisha kuwa ni pamoja na eneo husika liwe limetengwa kwa ajili ya matumizi ya makazi katika Mpango wa Jumla wa Jiji (Master Plan). 

 “Mpango huu ni shirikishi, wananchi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na wataalamu kubainisha mahitaji ya huduma za jamii na miundombinu na siyo makazi holela yote yana sifa ya kurasimishwa. “Alisisitiza Mlonda.

Aidha, alisema kuwa eneo husika ni lazima liwe na idadi kubwa ya watu wanaoishi katika eneo hilo ambao hawana uthibitisho wa uhalali wa kumiliki ardhi hata kama wanalipia ada. 

Kigezo kingine ni kuwepo kwa ongezeko kubwa la ujenzi wa nyumba katika eneo husika na idadi kubwa ya wakazi ambao wameishi katika eneo hilo kwa kipindi kirefu.

“Kuna maeneo mengi ambayo wamiliki wanaendelea kuuza mashamba au viwanja vyao na ujenzi wa nyumba mpya kwa ajili ya makazi na biashara unaendelea kwa kasi kubwa; ndio maana tumeona ni vyema tukaanza utaratibu huu wa kurasimisha ili watu wamiliki hayo maeneo kihalali.” Alifafanua Mlonda.

Pia idadi kubwa ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Asasi za Kijamii wamehamasika na wako tayari kushiriki katika mipango ya urasimishaji kwa kuchangia gharama za kupanga, kupima na kumilikisha.

Mlonda alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na viongozi wao wa Serikali za Mitaa kutatua migogoro ya mipaka na kutoa ardhi kwa ajili ya barabara kwani ndio msingi wa ufanisi katika zoezi la urasimishaji makazi. 

Makazi holela ni makazi ambayo yamejengwa bila kufuata Sheria, kanuni na taratibu za Mipangomiji. Ujenzi mijini unaongozwa na Sheria ya Mipangomiji namba 8 ya mwaka 2007 na ile ya Serikali za Mitaa sehemu ya mamlaka za miji ya mwaka 1982. ambazo zinaelekeza kupata kibali cha ujenzi kabla ya kujenga nyumba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...