Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inapenda kuujulisha umma kwamba mashine ya MRI itasimama kwa muda kufanya kazi baada ya kuharibika. Mashine hii iliharibiika tarehe 24/08/2016 baada ya kutokea hitilafu ya umeme.
Baada ya kuharibiika, tarehe hiyo (24/08/2016) mafundi wa Philips kwa kushirikiana na mafundi wetu walianza kutafuta athari baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme.
Tarehe 26/08/2016, mafundi walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hii kwa kuwa betri za awali zilikuwa zimefungwa muda mrefu. Tarehe 28/08/2016 mafundi walibaini kwamba kifaa cha Gradient Module kilikuwa kimeharibika na tayari hospitali kwa kushirikiana na Philips wameagiza kifaa hicho kutoka Uholanzi.
Hospitali ya Taifa Muhimbili inawaomba radhi wananchi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
Imetolewa na:
John Stephen, Ofisa Uhusiano,
Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja,
Hospitali ya Taifa Muhimbili
Tarehe 29/08/2016.
ETA lini? kitawafikia lini? maana mmeeleza kwamba mmeagiza au ndo hamjui kitawasili lini?
ReplyDeleteBack to square one
ReplyDeleteinapenda kuwajulisha au inasikitika kuwajulisha....?
ReplyDelete