Na
Abushehe Nondo na Sheila Simba - MAELEZO.
Serikali imesema
kuwa iliamua kununua ndege mbili za abiria aina ya Bombadier Q400 kutoka nchini
Canada kutokana na uhitaji wa huduma ya usafiri wa anga kwa safari za ndani ya
nchi na mazingira halisi ya viwanja vya ndege vilivyopo nchini.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani
katika chuo cha Taifa cha usafirishaji(NIT)
Mbarawa
alisema kuwa Serikali haikukurupuka katika kufanya maamuzi ya aina ya ndege za
kununua badala yake imezingatia vigezo na malengo mahsusi ya kuhudumia usafiri
wa ndani na kuboresha usafiri wa anga kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
“Serikali
imeamua kununua aina hii ya ndege za Bombadier Q400 kutokana na hali halisi ya
Viwanja vya ndege nchini kuwa vya Changarawe na lami kwa baadhi, huku lengo ni
kutoa huduma za usafiri wa ndani” Alisema Profesa Mbarawa.
Mbarawa
aliwataka Watanzania kuelewa nia ya Serikali yao ni kuhudumia wananchi hivyo
watu wasipotoshe ukweli kuhusu ndege hizo kwani zimezingatia mambo mbalimbali
ikiwemo suala la usalama na ufanisi katika uendeshaji wake.
Aliongeza
kuwa ndege hizo zina uwezo wa kutua katika viwanja vingi hapa nchini kwani zinaweza
kutua katika viwanja vyenye urefu wa kilomita 1.5 ambavyo ndio vingi nchini tofauti
na aina nyingine ambazo hutua kwenye viwanja vyenye urefu zaidi ya kilomita
mbili.
Prof.
Mbarawa alibainisha sababu nyingine kuwa ni aliongeza uwezo mdogo wa ndege hizo
katika kutumia mafuta ukilinganisha na aina zingine ambapo kwa safari ya kutoka
Dar es Salaam hadi Mwanza zitakuwa zikitumia Tani 1.7 za mafuta tofauti na aina
nyingine zinazotumia hadi Tani 2.8 kwa safari moja.
Waziri
Mbarawa pia alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulionezwa kuwa ndege hizo
zimenunuliwa katika kampuni ndogo isiyokuwa na sifa na kubainisha kuwa suala
hilo siyo la kweli kwani kampuni hiyo imefanya biashara na nchini nyingi
ikiwemo Ethiopia yenye ndege t19 aina ya Bombadier Q400 zilizotengezwa na Kampuni hiyo.
Mpaka
sasa tayari Serikali imeshafanya malipo ya ununuzi wa ndege hizo kwa asilimia
40 ambapo ndege hizo zinatarajiwa kuwasili nchi tarehe 19 septemba mwaka huu ambapo
zitaanza safari ya kutoka nchini Canada tarehe 15 septemba mwaka huu kupitia nchini
Uingereza.
Akizindua
mafunzo hayo ya wakufunzi wa marubani,
Waziri Mbarawa aliwaasa Marubani ambao watahitimu mafunzo hayo kuhakikisha wanazingatia suala na nidhamu na
uadilifu katika sekta hiyo ya usafiri wa anga.
“Hatutaki
kuwa na marubani ambao wana uwezo wa kazi lakini sio waadilifu,hakikisheni
mnawafundisha marubani wanafunzi kuzingatia nidhamu na uadilifu katika sekta
hiyo ya anga ambapo wakati mwingine Rubani anajijua anakasoro lakini bado
anang’ang’ania kurusha ndege” alisema Prof.Mbarawa.
Aidha
amesema kuwa Serikali itashirikiana na chuo hicho katika kutoa kozi za urubani
ili kuakabiliana na changamoto ya ukosefu wa marubani nchini.
Ni wazo zuri la kufufua Air Tanzania. lakini muhimu ili ishindane na mashirika mengine ya ndani inahitajika kuwa na ndege zenye engine ya jet,na kubwa kidogo kushindana na fastjet ambao wanandege kubwa za uwezo wa kubeba abiria 150 na hii inakwenda Mwanza kwa saa moja wakati hizi za propeller engine ni masaa 2,mimi nafikiri inatakiwa kuwa na CRJ 200 ambazo watengenezaji ni hao hao na zinachukua abiria 50 lakini jet engine.lakini naunga mkono kwa asilimia mia bora kuwa na chetu lakini tatizo watendaji je watatunyanyua???
ReplyDeletekupanda panga hilo, aah
ReplyDeleteThe mdudu, safi sana awamu ya 5 chini ya Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli na serikali yake yote kwa ujumla mdogo mdogo tutafika mpaka kwenye ma hayo ma Boeing ila minaona zingekuwa chini ya management ya mashilika kama NSSF au PPF kwa sababu haya mashilika tunaziona kazi wanazo zifanya kwakua wapo makini sana
ReplyDeleteMtoa maoni wa kwanza, kukujibu ushauri wako. Umwshamsikia Mh. Magufuli kasema mwakani 2017 Airbus mbili zitanunuliwa, hizo sio za "pangaboy"
ReplyDeleteJamaa anakwenda na hesabu zake. Sasa huko Newala utapeleka Jet engine???
Kuweni na subira kidogo, miaka 30 imekwenda ATC inasota tu, jamaa anataka kufufua mnaaza kulaumu aina za ndege.
Ahsanteni.
Mdau MD
Safi sana, hivyo ndivyo tusonge mbele TANZANIA OYEE!!!
ReplyDeleteKweli kabisa wadau tunaanza humu humu mwetu kwanza. Tatizo letu watz hatusikilizi na kutunza maneno ya ahadi au SERA ili utekezaji ukianza tusiwe wa kushangaa. JPM anaanzia chini kwenda juu au anaanzia ndani kwenda nje ya nchi. Hivyo tuwe na subira ambayo ina heri. Amekuja bwana kupanga na kutekeleza kwa uwazi sasa lawama za nini? . TUSUBIRI KIDOGO, boeing tutanunuatu.
ReplyDeleteMaelezo ya professa - waziri husuka aliyoyatoa juzi yapo wazi na yanajitosheleza (kasema kwa kuanzia tunanaza na ndege zenye uwezo wa kutua viwanja vingi na ambazo ni lahisi keudeshwa na shirika linalofufuka, break even inafikiwa na abilia 26 sasa ndege kubwa ukaipeleka kwa watani zangu Kigoma break even abilia 65 utawapata kila siku? hivyo ni sawa kabisa kuanza na hizo,wanaangalia capacity na soko lililopo vilevile miundo mbinu...tembeleane tovuti za mashirika makubwa kwenye fleet zao utaona hizo unazosema panga wanazitumia pia eg Ethiopian airline
ReplyDelete