Waandishi wa habari 17 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini China ikiwemo cctv wakiongozwa na balozi Liu Guzjin wapo hapa nchini kwa ziara ya siku nne ambapo jana walitembelea hifadhi ya Taifa ya Mikumi na kuvutiwa na wanyama wa aina mbalimbali wakiwemo  tembo, simba, makundi ya nyati na wengineo wanaopatikana katika hifadhi hiyo.
Aidha waandishi hao wa habari walivutiwa pia na ukarimu wa watanzania kwa ujumla na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania kama eneo bora la Utalii barani Afrika kwa wananchi wa China kupitia katika vyombo vyao vya habri wanavyofanyia kazi.
“Tumefurahishwa kuona wanyama wa kuvutia miongoni mwao wakiwemo wale maarufu watano lakini pia na ukarimu wa watu wa Tanzania, na kwa kweli watanzania ni rafiki zetu. Tunaahidi takuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania kwa ndugu zetu nchini China.” Alisema  Balozi Liu. Ameongeza kuwa Tanzania ni nchi yenye vivutio vizuri vya utalii ambavyo hapana shaka kabisa wachina wengi watapenda kuja kuvitembelea na kuviona.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) Bw. Allan Kijazi aliwaambia wandishi hao muda mfupi baada ya waandishi hao kutembelea hifadhi hiyo kuwa Shirika lake limejipanga vema katika kuimarisha uhifadhi wa wanyama na vivutio vingine vya utalii vilivyo ndani ya hifadhi zote za Taifa pamoja na mazingira yake kwa lengo la kuhakikisha kuwa utalii unakuwa endelevu.
Naye AfisaUuhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Geofrey Tengeneza akizungumza ujio wa waandishi hawa kutoka China utasaidia katika kuitangaza sana Tanzania kama eneo la utalii kwa watu wa China na hasa ikizingatiwa kuwa soko la China ni miongoni mwa masoko yanayolengwa sana na TTB kupitia mpango wake mkakati wa utangazaji utalii Kimataifa. 
Pamoja na mambo mengine waandishi hao walitarajiwa  pia jana kutembelea kituo cha Kilimo  kinachoendeshwa na China kilichoko Morogoro na kutoa msaada wa vifaa vya kilimo. Aidha leo waandishi hao wanatarajia kushiriki katika mkutano wa Kimataifa baina ya China na Afrika kujadili maendeleo ya kidiplomasia utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es salaam. 
 Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Bw. Allan Kijazi akizungumza na waandishi wa habari wa China katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi mara baada ya kutembelea hifadhi hiyo..
 Afisa Uhusiano Mkuu wa TTB Bw. Geofrey Tengeneza akizungumza na mkuu wa msafara wa waandishi wa habari kutoka China balozi Liu Guzjin muda mfupi kabla balozi huyo hajakabidhiwa DVDs na machapisho ya TTB yanayoelezea vivutio vya utalii wa Tanzania.
Waandishi wa habari kutoka China wakiongozwa na balozi Liu Guzjin (wa tano kushoto aliyenyoosha mkono)  wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa TANAPA Bw. Allan Kijazi (wa tano kushoto walio simama), Afisa Uhusiano Mkuu wa TTB Bw. Geofrey Tengeneza (wa tano kulia waliosimama) na maafisa wa hifadhi ya Mikumi muda mfupi baada ya waandishi hao kutoka China kuwasili katika hifadhi ya Mikumi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...