Kampuni ya mawasiliano ya
Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na WIzara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeanzisha na kuzindua namba
maalumu kwa watanzania kuchangia ili kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi
lililotokea mnamo tarehe 10 Septemba 2016 majira ya mchana huko Bukoba mkoani
kagera. Watu 17 wamepoteza maisha na kuacha mamia wakiwa hawana makazi kufuatia
tetemeko hilo.
Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja Huduma za jamii Hawa Bayumi
alisema, “Tunaungana kwa pamoja katika maafa haya na kutoa pole kwa familia
zilizopoteza ndugu na wanafamilia kutokana na tetemeko hili pia limewaacha
mamia wakiwa hawana makazi. Leo tunaungana na wakazi wa Kagera katika
janga hili kwa kutoa mchango kwa waathirika wa tetemeko na kuwaomba watanzania
wote kuungana nasi kwa kuchangia kupitia namba maalumu 155990 itakayotumika
kuchangisha fedha kwa ajili ya waathirika wa janga hili wanaohitaji msaada wa
haraka.
Jinsi ya kuchangia ni rahisi,
1.
unapiga *150*60# kuingia kwenye airtel money
2.
unachagua 5 yaani lipa bili kwa Airtel Money,
3.
kisha unachagua 4 andika jina la biashara ambapo
utaandika 155990,
4.
Kisha ingiza kiasi cha fedha unachotaka kuchangia
5.
Weka kumbukumbu namba ambayo ni jina lako
6.
Kisha malizia kwa kuweka namba ya siri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...